Kabila la Wachaga linapatikana mkoani Kilimanjaro. Kwa
asili, Wachaga ni mchanganyiko wa Wamasai,
Wasambaa, Wataita, Wakamba na Wakahe.
Wachaga walianza kuhamia kwenye miteremko
ya Mlima Kilimanjaro kwenye karne ya 17.
Wachagga ni kabila la watu wenye asili ya Kibantu lakini pia mchanganyiko wa damu, hasa ya Kikushi wanaoishi kaskazini mwa Tanzania chini ya mlima Kilimanjaro, mkoani Kilimanjaro.Shughuli kubwa ya Wachagga ni biashara na kilimo.Wachagga ni kabila la tatu kwa ukubwa nchini Tanzania. Takwimu za mwaka 2003 zinaonyesha kuwa idadi ya Wachagga 2,000,000.
TABIA ZA WACHAGA.......
Wachaga wamegawanyika kama ifuatavyo, sio
wote wajanja. Kuna:-
1. WAROMBO; Hawa wajanja sana kibiashara/
wezi pia. wanapenda dili za magendo. Ni walevi
sana hupeleka wake zao vijijini wakileta kiburi
mjini. Wanaume wa Rombo wanachunwa sana
na wanawake wa Marangu na wanawaita
"vishohia". Wanawake wa Rombo ni mama
Huruma, wanaachia tu.. Ukioa Mrombo ujue
umeolea kijiji.
2. WAMARANGU; Ni wazuri sana wa sura na
umbo, wanavutia. Lakini wanawachuna sana
Warombo. Wanawake wa Marangu wana dharau
sana na wanaume ni waoga kuliko wanawake.
Mwanaume wa Marangu kupigwa na mkewe si
jambo la ajabu.
3. WAKIBOSHO; wanafanana na Warombo
lakini ni wavumilivu zaidi. Biashara kubwa
wanayofanya ni ya kuchinja... wengi wanamiliki
mabucha. Wana hasira sana na ni wakatili..
Akikuchoma kisu, siku ya mazishi anakuja kudai
kisu chake.
4. WAMACHAME; hawa ni wezi sana, ukifanya
nae dili umeliwa. Ni wasiri sana lakini wako
makini mno hasa kwenye pesa. Wakiwa na
hasira hawaoneshi waziwazi, so Mmachame
anaweza kukuua huku akitabasamu. Sio
waaminifu sana lakini wanaenda kanisani mara
nyingi zaidi kuliko Wachaga wote. Wanawake
wa machame wanaitwa 'Wapalestina'.. Mume
ukitajirika mkeo anakuua ili arithi mali.
5. WAURU; hawa hupenda kusoma sana lakini
hawapendi maendeleo kabisa. Hadi leo eneo
lao la Kishumundu linatumika ku-identify
wachagga washamba. Wanawake wakifikisha
umri wa miaka 40 hua wehu na wanaume huwa
vichaa mapema zaidi. Wanaume ni wavivu,
lakini wanawake ni wachapakazi hodari.
Wanazurura mjini na mabeseni wakiuza ndizi
mbivu.. Ukioa Uru jiandae kulea kichaa.
6. WASIHA; Kwanza hawapendi kuitwa
Wachagga. Wanajiita watu wa West-Kilimanjar
o. Ni mchanganyiko wa Wachagga na WaMeru.
Hawapendi shule ila wanapenda zaidi kazi za
ufundi na kilimo. Viazi vingi vya Chips Arusha
na Moshi vinatoka kwao. Wanawake zao wana
"vigimbi" mguuni sababu ya kulima mno.!
7. WAKIRUA; wanapenda sifa kama Wahaya.
Vikundi vya Wachagga
Wachagga wana historia ndefu ya asili yao na ya maingiliano yao na makabila mengine. Kabila la Kichagga ni mkusanyiko wa makabila madogomadogo (ya Kichagga) yaliyosambaa kijiografia kuzunguka mlima Kilimanjaro kuanzia mashariki (Tarakea, Rombo) hadi magharibi kwa Kilimanjaro (Siha, Machame).
Makabila ya Kichagga ni Wa-Rombo, Wa-Vunjo ambao wanajumuisha watu wa Mwika, Mamba, Marangu, Kilema na Kirua ambayo ndio inajulikana na wengi kama Kirua Vunjo. Ukipenda unaweza kuwagawa watu hawa wa Vunjo kama Wa-Mwika, Wa-Mamba ,Wa-Marangu,Wa-Kilema,na Wakirua.Makabil
a mengine ni Wa-Old Moshi, Wa-Kibosho, na Wa-Machame, Wa-Uru, na Wa-Siha.
Watu wengi wanafikiria kwamba Wachaga
wanatokana na asili moja. Ukweli ni kwamba
wamegawanyika katika himaya 15,
wanatofautiana kwa lafudhi, lugha, rangi na
mwonekano wa miili yao. Wachaga wapo katika
makundi makuu matatu ya Hai, Vunjo na
Rombo.
Wale wanaopatikana eneo la Hai ni Wasiha,
Wamasama, Wamachame,Wangíuni, Wakibosho,
Wauru na Wamoshi. Kwa wale wanaopatikana
eneo la Vunjo ni Wakirua, Wakilema,
Wamarangu, Wamamba na Wamwika.
Kutoka eneo la Rombo ni Wamkuu, Wamashati
na Wasseri.
Hadi sasa haijulikani vizuri asili ya jina
Wachaga, ila wanahistoria wanaeleza kwamba
jina hilo linatokana na neno la Kiswahili
linaloitwa 'Kichaka'.
Inaelezwa kwamba misafara ya
wafanyabiashara iliyokuwa ikiongozwa na
Waswahili pamoja na Waarabu, walipokuwa
wakipita maeneo ya Vunjo waliwaona wenyeji
wa huko wakiwa wamejenga vibanda vya
kulinda mazao yao yasiliwe na wanyama
waharibifu.
Wakawaita wenyeji hawa kwamba wanaishi
vichakani na kuanzia hapo wageni
wafanyabiashara na Wamisionari walipokuwa
wanakuja Kilimanjaro walielekezwa na
waongozaji misafara yao kwamba wanakwenda
kwenye nchi ya “Uchakani”, wakimaanisha
kwamba kwa watu wanaoishi vichakani.
Hatimaye wageni wakashindwa kulitamka vizuri
neno hili na kuliita ìUchagani,
Jina hili likawekwa kwenye ramani na kuitwa
nchi ya “Wachaga”. Hivyo ndivyo wenyeji
waliokuwa wakiishi kwenye Miteremko ya Mlima
Kilimanjaro walivyopewa jina lao. Wachaga.
Maendeleo ya Wachaga
Maendeleo yao hapo awali yalitokana na zao la
kahawa. Walifanikiwa kuanzisha vyama vya
ushirika na hatimaye mwaka 1932 walianzisha
Halmashauri ya Wachaga (Chaga Council)
ambayo kwa sasa inatumiwa na Halmashauri
ya Wilaya ya Moshi. Halmashauri hii iliongozwa
na Mangi Mkuu Mshumbue Thomas Marealle II.
Mwaka 1946, utawala wa Waingereza
uliboresha Baraza la Halmashauri ya Wachaga.
Himaya ndogo za Wachaga zipatazo 17
(himaya mbili za Wakahe na Waarusha chini
zilijumuishwa kwenye Tarafa ya Vunjo) na
kuundwa kwa Tarafa tatu za Hai, Vunjo na
Rombo.
Halmashauri ya Wachaga ilijenga miundombinu
na huduma za jamii ikiwamo kuwasomesha
watoto wao kwenye shule na vyuo mbalimbali
kama Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda.
Halmashauri ya Uchaga ilikuwa na bendera
yake ambayo ipo hadi leo kwenye Halmashauri
ya Wilaya ya Moshi, yenye nembo tano kuu:
1. Mlima Kilimanjaro uliochorwa katikati ya
bendera ukionyesha mandhari nzuri ya kilele
cha Kibo. Kilele cha Kibo kinatoa maji safi na ni
kielelezo cha umoja wao.
2. Chini ya kilele cha Kibo, upande wa kushoto
wa bendera kuna mgomba wenye ndizi. Hiki ni
chakula kikuu cha Wachaga.
3. Upande wa kulia wa bendera ni tawi la mbuni
ukiwa na matunda yake. Kahawa ni zao
lililowaletea maendeleo.
4. Bendera imezungukwa na matawi ya 'sale'
lenye matawi mawili (draceana plant). Matawi
haya yamefanya mduara kuzunguka kilele cha
Kibo, mgomba wa ndizi na tawi la zao la
kahawa. Masale ni mmea unaoheshimiwa sana
na Wachaga wote.
Ni alama ya amani. Masale hutumika katika
sherehe na shughuli zote za kimila
zinazofanywa na Wachaga. Majani yake ni
kijani kibichi yanayoonyesha jinsi Kilimanjaro
ilivyo na rutuba nzuri inayostawisha mazao ya
kila aina.
5. Juu kidogo ya kilele cha Kibo yupo chui
ambaye amejipumzisha. Chui ni alama kuu ya
mamlaka ya Wachaga.
Hapo awali kwenye miteremko ya Mlima
Kilimanjaro walikuwepo chui wengi wa rangi
nyeusi lakini kutokana na ongezeko la watu
pamoja na uharibifu wa mazingira chui hawa
wametoweka.
Sikukuu ya Wachaga
Sikukuu ya Wachaga wote ilikuwa
ikiadhimishwa Novemba 10 kila mwaka kama
kumbukumbu ya siku ambayo Wachaga wote
walipokusanyika na kumchagua Mangi Mkuu
baada ya kuteuliwa na Halmashauri Kuu ya
Uchaga.
Maadhimisho ya kwanza ya mwaka 1952
yalitanguliwa na uchaguzi wa Halmashauri ya
Wachaga wote kuanzia kwenye ngazi ya Uchili
(kijiji), Umangi ( uchifu wa eneo) na mwisho
ngazi ya baraza kuu.
WAJUE WACHAGGA
Lugha ya Kichagga
Lugha ya Kichagga inabadilika kuanzia unapotoka Tarakea mpaka unapofika Siha magharibi mwa Kilimanjaro.
Kutokana na tofauti hizo Kichagga kimegawanyika katika Kirombo, Kivunjo, Ki-Old Moshi, Kiuru,Kikibosho, Kimachame, na Kisiha.
Lugha hizo zinakaribia kufanana kadiri makabila hayo yalivyopakana. Kwa mfano, Kivunjo kinafanana na Ki-Old Moshi. Vile vile Kisiha kinafanana sana na Kimachame ambacho pia kinafanana kidogo na Kikibosho.
Baadhi ya Wamachame walihamia sehemu za Meru, Arusha, na kuchanganyikana na Waarusha, lugha yao ikabadilika kidogo na kuwa Kimeru. Kwa sababu hiyo Wameru wanasikilizana sana na Wamachame ingawa lafudhi zao zinatofautiana kidogo.
Historia ya elimu kati ya Wachagga
Wachagga wanajulikana kwa uwezo wao mkubwa wa kufanya biashara na pia kilimo. Moshi ni maeneo ya mwanzo ambayo Wamisionari wa Ukristo walijenga makanisa na shule.
Sababu hii imefanya Wachagga kuwa kabila lenye watu wengi zaidi walio na elimu ya kisasa na mkoa wa Kilimanjaro unaongoza kwa idadi ya shule za sekondari nchini Tanzania. Kulingana na takwimu za elimu mkoa wa Kilimanjaro una shule za sekondari zaidi ya 320. Pia mkoa una shule za msingi zipatazo 950. Idadi hii ya shule ni kubwa zaidi ya idadi ya shule katika mikoa mingine Tanzania.
Shule nyingi za sekondari ziko katika mkoa huu kwa sababu zifuatazo: 1) Hali ya hewa na vivutio vya kitalii katika mkoa huu viliwavutia zaidi walowezi na wakoloni na kuweka makazi yao hapo. Hivyo wamisionari walijenga shule za kwanza wakifuatiliwa na serikali za wakoloni 2) Serikali ya Tanzania ilirithi shule zilizojengwa na wakoloni 3) Wachagga waliobahatika kupata fedha binafsi baadaye waliwekeza kwenye ujenzi wa shule binafsi kama kitega-uchumi, wakati wakazi wa mikoa mingine kadhaa walisubiri serikali iwajengee shule. 4) Ukichanganya sababu 1, 2 & 3 utagundua shule katika mkoa Kilimanjaro zimezidi sana idadi ya shule katika mikoa mingine yote.
Ni vema pia kusema kUwa shule hizo huvutia wanafunzi kutoka Tanzania nzima, haziwasomeshi Wachagga tu.
Kilimo na chakula
Wachagga hulima mazao ya chakula kama vile mahindi, maharagwe, viazi, ndizi, ulezi na mboga mbalimbali. Pia mazao ya biashara kama vile kahawa, nyanya na vitunguu.
Ndizi za Wachagga
Ingawa Wachagga wa leo wanakula vyakula mbalimbali kama vile ugali, wali na viazi, chakula kikuu cha Wachagga ni ndizi.
Kuna ndizi za aina mbalimbali na kwa matumizi tofauti. Mfano ndizi sukari ni fupi na huachwa hadi ziive na huliwa mbivu kama tunda.
Ndizi mshale hukatwa zikiwa mbichi na kupikiwa vyakula mbalimbali pamoja na nyama ya ng'ombe, kondoo au mbuzi. Mara nyingine hupikwa na maharage, choroko, kunde au hata maziwa ya mtindi. Vyakula vya ndizi huja kwa ladha tofauti kama vile ndizi nyama, mtori, machalari, kiburu na kadhalika.
Aina nyingine ni ndizi ng'ombe ambazo huachwa ziive halafu humenywa na kutumiwa kutengenezea pombe maarufu iitwayo mbege. Mbege hutengenezwa kwa kutumia ndizi mbivu, maji, na ulezi.
Aina nyingine ni ndizi mzuzu. Hizi zikikomaa huachwa zianze kuiva kidogo halafu huchomwa na kuliwa kama kitafunwa pamoja na chai au pombe. Ukipita mitaa ya Dar es Salaam utaona ndizi mzuzu zikichomwa sambamba na muhogo au kuku vumbi au kiti moto.
Wachagga na muhogo
Inasemekana kuwa "Mchagga halisi hali muhogo - akila muhogo atakufa". Usemi huu umetokana na historia ya mababu kuwa Wachagga waliopanda mihogo Kilimanjaro enzi za kale walikufa baada ya kuila. Historia hiyo yaweza kuwa ya ukweli kwa sababu aina nyingi za mihogo zinajenga sumu ya sianidi ndani yake; watu waliozoea kutumia mihogo huwa na njia za kuondoa sumu kwa kuiloweka mihogo katika maji kwa muda. Lakini kama Wachagga wale wa zamani, hasa wa Machame, walifanya jaribio bila kujua mbinu ya kuondoa sumu, ajali iliweza kutokea. Cha kushangaza ni kwamba hukohuko Kilimanjaro, majirani na watani wa Wachagga, yaani Wapare, walikuwa wameshazoea mihogo na ilikuja kuwa moja ya chakula chao kikuu.
Ulaji kiti-moto
Pamoja na kilimo cha mazao, Wachagga hupendelea sana kufuga nguruwe. Tabia ya kula nyama ya nguruwe ijulikanayo leo kwa jina la "kiti moto" ni moja ya mambo yaliyoenezwa na Wachagga. Ulaji wa "kiti moto" haukuwa pendeza baadhi ya wenyeji wa Pwani kama Dar es Salaam ambapo Wachagga walihamia, kwani wakaaji wengi wa Pwani ni Waislamu kwa hiyo nguruwe kwao ni haramu. Wakazi wa Dar es Salaam watokao makabila mengine na wasiyo Waislamu kwao kula nguruwe ilikuwa "ruksa".
Ni matumaini yangu kwamba umegundua kitu kupitia historia hii murua ya wachaga,
Nakutakia siku Njema, Mungu Akubariki na kukulinda
إرسال تعليق