Samsung wako mbioni kuja na teknolojia mpya  ya Betri za simu itakayopunguza gharama za utengenezaji wa betri mpya zitakazokuwa zinadumu na chaji kuliko zinazotumika sasa.
 
Teknolojia hiyo mpya waliyokuja nayo inafanya betri ya simu iweze kudumu muda mrefu kwa matumizi mengi baada ya kuchaji ukilinganisha na ubora wa betri zinazotengenezwa kwa teknolojia inayotumika sasa.
 
Samsung walitambulisha rasmi ugunduzi wa teknolojia yao mwaka 2004 ila hadi sasa wanafanya utafiti zaidi kuhakikisha ubora, usalama na uwezo wa kutengeneza betri hizo.
 
Hadi sasa changamoto wanayopambana nayo ni kupunguza gharama zinazotumika katika uzalishaji wa betri hizi. 

Kwa wastani imeonekana teknolojia hiyo ina wastani wa gharama kubwa kwa kila utengenezaji wa betri moja ukilinganisha na betri zinazotumika kwa sasa.

Post a Comment

Previous Post Next Post