Wananchi wa kijiji cha Bwai wilayani Musoma vijijini mkoani Mara' wameharibu na kujaribu kulichoma moto gari la polisi baada ya polisi kuwazuia kumshambulia mwalimu Lazaro Mmanga ambae pia ni kaimu mkuu wa shule ya msingi Bwai aliyekuwa akishambuliwa na wananchi hao baada ya kukutwa amejifungia ofisini na mwanafunzi wa kike wa darasa la saba (Jina linahifadhiwa) ambae taarifa za awali zinadai wawili hao walikuwa wakifanya mapenzi ofisini Kwa mwalimu huyo.Taarifa za kujifungia ofisini Kwa mwalimu na mwanafunzi huyo zilitolewa na wanafunzi wa shule hiyo ambao pia walieleza kuwa si mara ya kwanza Kwa wawili hao kujifungia ofisini.

Kamanda wa Polisi mkoani Mara ACP Juma Ndaki amethibitisha kutokea Kwa tukio hilo hapo jana jumatano.

Post a Comment

Previous Post Next Post