Nilibahatika kutembelea Toulouse, Ufaransa, kujionea kiwanda cha kampuni ya Airbus ya kuundia ndege. Ila nimestuka kusikia kwamba Kampuni ya Airbus imetangaza kwamba itasitisha uundwaji wa ndege zake kubwa za abiria za A380 baada ya mteja wake mkuu Emirates Airline kupunguza oda ya ndege mpya 39.
Baada ya kuwekeza sana kwenye ndege hiyo ya A380, kampuni hiyo kubwa kuliko zote za Ulaya ilitegemea kumshinda mshindani wake mkuu anayetamba kwa ndege yake ya Boeing 747. Lakini wateja wameonekana kutamani ndege ndogo zaidi ambazo gharama ya uendeshaji ni ndogo.
Kampuni hii ndiyo inayounda na kuuza ndege kubwa kuliko zote za abiria za A380, wakati ndege yake ya 10,000, aina ya A350, imenunuliwa mwaka juzi na Singapore Airlines. Kwa jumla ndege za Airbus zimefanya safari milioni 110, ambazo ni kilometa bilioni 215 na kubeba abiria bilioni 12.
Kati ya mwaka 2000 hado 2014 kampuni ya Airbus ilijulikana kama European Aeronautic Defence and Space Company (EADS), ikiwa ni shirika la Ulaya likiwa limesajiliwa Uholanzi na kuwa na hisa za kibiashara na Ufaransa, Ujerumani na Hispania. Shughuli yake kuu ni kuunda na kuuza vifaa vya anga duniani kote, ikiwa na divisheni tatu za kuunda na kuuza ndege za kibiashara, ulinzi na anga na helikopta.
Shughuli kuu za uundaji wa ndege za biashara zipo mjini Blagnac, Ufaransa, kwenye kitongoji cha mji wa Toulouse, wakati shughuli za uundaji na uzalishaji wake zikiwa Ulaya (Ufaransa, Ujerumani, Spain na Uingereza) na pia nchini China na Marekani.
Sehemu kuu za mwisho za kuunganisha ndege zipo Toulouse, Ufaransa, Hamburg, Ujerumani, Seville, Spain, Tianjin, China na Mobile, Alabama, Marekani.
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) lina ndege mbili aina ya Airbus A22-300 ambazo pamoja na Beoing 787 Dreamliner zililetw3a kati ya mwezi Mei na Desemba mwaka 2018.
Kabla ya hapo ndege mbili za Bombadier CASH8 Q400 zililetwa Septemba 2016 na ingine Juni 2017. Hadi Julai mwaka jana shirika hilo lilikuwa linaendesha kazi kwa ndege saba, ikiwemo Bombadier DASG8 Q300 iliyokuwa ikitoa huduma tangia mwaka 2011.
Post a Comment