ABIRIA 35 na wahudumu 12 wamenusurika kifo mapema leo Ijumaa baada ya ndege waliokuwa wakisafiria kukosea njia na kuanguka katikati ya Bahari ya Pacific katika Kisiwa cha Micronesia.





Abiria wote katika ndege hiyo ya Shirika la Ndege la New Guinea (Air Niugini), ANG73 aina ya Boeing 737 – 800 wamepelekwa hospitalini kwa uchunguzi na matibabu.





Imeelezwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni upepo mkali na hali ya hewa kubadilika ghafla ambapo ilianza kunyesha mvua kubwa muda mfupi baada ya kupaa jambo lililosababisha ndege hiyo kupotea njia na ilipojaribu kutua katika Uwanja wa Kimataifa wa Chuuk, ilianguka baharini.



Imeelezwa pia kuwa, baada ya ajali hiyo kutokea na ndege kuanguka majini, abiria na wahudumu wa ndege hiyo walipitia mlango wa dharura wa ndege kabla ya kuokolewa.

Post a Comment

أحدث أقدم