Wahaya walitokea Afrika Kaskazini na kupitia Uganda na hatimaye kuanza maisha katika eneo la Kagera kaskazini magharibi mwa Tanzania
Wahaya ni moja ya makabila yaliyojaliwa wanawake wazuri na wenye maumbo na shepu nzuri pamoja na tabia.
Lugha, Tamaduni,chakula (Ndizi) ya watu wa kabila hili inafanana sana na ile ya jamii ya wanyankole wa nchi jirani ya Uganda
Wahaya walianza kutambiana toka zamani na kigezo kikubwa ilikuwa ni kuwa na elimu bora “inye nsomile” maana ya “Mimi nimesoma” na huu ukawa mwanzo wa makabila mengine kuwaita “NSHOMILE”
Wahaya ni mkusanyiko wa makabila saba,ambayo ni
waziba,
wahamba
wanyambo,
wanyaiyangilo,
wayoza
waendangabo
wakala.
Ni mkusanyiko kwa maana haya ni makabila kamili sio makabila madogo madogo kama watu wengi wanavyofikiria.
Hayo makabila kila moja ilikuwa ni dola kamili iliyokuwa na mamlaka kamili katika nyanja zote za kiutawala,kijamii,kisiasa kiuchumi na kijeshi.Na kila dola lilikuwa na mipaka isiyoingiliana na dola jingine na iliyolindwa barabara.
Senene ni chakula cha heshima kwa wahaya toka zama za kale
Jamii hii ilikuwa na utawala wa wa koo na mtawala mkuu aliitwa Mukama
Alitokana na ukoo maalumu uliotoa mukama kila dola ilikuwa na koo tofauti zilizizotoa Bakama,Waziba ukoo uliotoa
Bakama ni ukoo wa Babiito.Wanyambo,Wanyaiyangilo na Wahamba ukoo wa Bakama ni Bahinda.
Hawa watawala walikuwa na mamlaka kamili kila mmoja kwenye dola lake bila kutegemea mtawala wa dola jirani.Mara nyingi dola hizi zilikuwa na migogoro ya mipaka iliyopelekea kutokea vita baina ya dola moja na nyingine.
Lugha za kila kabila zilifanana sana isipokuwa kulikuwepo na tofauti kubwa katika lahaja na tofauti ya baadhi ya maneno mfano maharage waziba na wanyambo wanaita biimba na makabila mengine wanaita mpelege. Pia kuna tofauti katka mila na desturi kutoka kabila moja na kabila jingine.
Kwa asili hakuna kabila mojalinaloitwa wahaya,hili jina limeundwa na wakoloni wa kijerumani.Wamekusanya makabila saba yenye lugha, mila na desturi zinazoshabihiana wakaliita kabila mmoja wahaya.Kwa kawaida kila kabila huwa lina mtemi wake au kiongozi mkuu wa kabila kwa kabila hili lililoitwa wahaya halina kiongozi wa aina hiyo.
MAJINA YA WAHAYA
Mtoto wa kwanza anaweza kuitwa Kokubanza, kokutangilila, Lubanzibwa Kalimuna
kama mtoto angezaliwa baada ya wazazi kukaa muda mrefu bila kupata mtoto, mtoto aliyezaliwa aliitwa ama Mushumbusi, Shumbusho, Rwezaula, kukulingilila, kokumalamala au Mkaanguki
Kama baba angekufa akamwacha mke wake ana mimba, mtoto aliyezaliwa aliitwa Kabwanga wa kike, kasigwa au kashangaki wa kiume
Pacha wa kiume aliyezaliwa kwanza aliitwa Ishengoma au Kakulu wa kike aliitwa Nyangoma, Pacha wapili kama ni wakiume aliitwa Kato. Wa kike alitwa Nyakato
Mtoto aliyezaliwa akiwafuata mapacha wakiume aliitwa Kyaluzi wa kike aliitwa Mkabaluzi
Kwa wahaya mapacha si tu watoto wanaozaliwa wawili, hata mtoto mmoja anayezaliwa kwa kutanguliza miguu huitwa pacha tena huyu ndiye huitwa pacha halisi. Kwa wahaya huita ‘eilongo alikulu’
Majina mengi ya kike huanza na KOKU mfano Kokushubila, kukoshobokelwa, Kokugonza nay a kiume huanza na Ruta kama Lutakulembelwa, Lutanywana, Lutasingwa
Kuna matumizi ya herufi ya R na H katika lugha ya luhaya sijayaelewa vizuri maana katika kuongea kwa wahaya uwezi kusikia mtu anajiita muhaya utamsikia anajiita muaya, utasikia anajiita Lweyemamu sio Rweyemamu
Wanawake wa Kihaya hutakiwa kulima heka za Maharagwe kwa ajili ya matumizi ya kaya yake na hawapaswi kusaidiwa na mumewe hata kama ni heka 10
[1/7, 8:40 AM] Rev.Prof.Ketaro: HISTORIA YA KIANTHROPOLOJIA NA KIFILOLOJIA KUHUSU ZILIZOKUWA KOO ZA WAGANDA NA WAHAYA KUANZIA MWAKA WA 2000 KK:
ردحذفKoo za Wahaya na Waganda ni koo zilizotokana na uzao wa aliyekuwa dada wa Mfalme Sheba bin Raama bin Kushi aliyeitwa kwa lugha ya Kibantu "Haiya" kwa maana ya "Pazuri". Lakini hata hivyo,wao Wanailoti wa jamii ya Waluo wao walimwita mama huyo kwa lugha ya Kinailoti "Waya" kwa maana ya "Shangazi".
Huyo Haiya baadaye alizaa mtoto ambaye aliitwa kwa jina la Kibantu "Ganda" kwa maana ya "Ya-tumbo". Inasimuliwa kuwa mama huyo alimwita mwanaye huyo kwa jina hilo kwa kuwa alitamani sana awe mtaalamu wa maswala ya tiba ya tumbo ambapo baada ya kuwa mkubwa alipelekwa mlima Rorya kulipokuwa na Wataalamu wa tiba za asili kufundishwa mambo ya tiba na uganga.
Hivyo basi, kutokana na masimulizi ya kale ya kietimolojia na Kifilolojia inaonyesha kuwa huyo mama aliyeitwa Haiya/Waya alikuwa ni binti Raama bin Kushi, kwa maana kwamba alikuwa ni dada wa Mflame Sheba aliyetawala upande wote wa Kusini mwa nchi ya Kushi (Kusini mwa Bara la Afrika) kuanzia mwaka wa 2200 KK.
Hivyo basi, hadi kufikia miaka ya 2000 KK watu wa uzao wa Haiya na Ganda walikuwa wamezaliana na kuwa koo kubwa kabisa ambazo hatua kwa hatua walisafiri na kuenea hadi maeneo ya Kigoma ambako koo hizo mbili kuu ziliitwa kwa lugha ya Kibantu "Abahaiya" kwa maana ya "Watu wa Pazuri" na "Abaganda" kwa maana ya "Watu walihusika na timba za magonjwa ya tumbo".
Hivyo basi,hapo Kigoma ambapo tafsiri yake kwa lugha ya Kibantu cha kale ni "Maasi",koo hizo mbili kubwa za Wabatu zilifarakana kwa sababu ya kugombea maeneo ambapo kwa ajili ya kufanya shughuli za kilimo Wabantu wa kutoka koo ya Abahaiya (Wahaya) walifieka maeneo ya misitu iliyotegemewa na Wabantu wa kutoka koo ya Abaganda (Waganda) kwa ajili ya shughuli zao za utabibu.
Hivyo basi, kutokana na kuzuka mgogoro huo, koo hizo ziliingia katika mafarakano yalizua ungomvi mkubwa na kusababisha maasi ya kikoo ambapo koo hizo mbili kubwa zilitengana na hivyo eneo hilo walikotengana likaitwa "Kigoma" kwa maana ya "Maasi" ambapo kutokea hapo Kigoma koo ya Abahaiya (Wahaya) ilijielekeza kukaa upande wa Bukoba kukabili Ziwa Victoria na koo ya Abaganda (Waganda) nayo ikajielekeza kukaa upande wa Uganda kukabili Ziwa Victoria pia na kumaliza ugomvi wao.
[1/7, 8:51 AM] Rev.Prof.Ketaro: Kwa hiyo basi, zamani hizo kwa lugha ya Kibantu iliyotumika kwa wakati huo nchi ya Uganda iliitwa "Boganda" na ilipozaliwa lugha ya Kiswahili ikaitwa "Uganda" na halikadhalika hapo kale kabla ya kuja kwa lugha hiyo ya Kiswahili kulikuwa na Abahaiya/Abahaya na baada ya kuzaliwa kwa lugha ya Kiswahili wakaitwa , "Wahaiya/Wahaya".
[1/7, 8:56 AM] Rev.Prof.Ketaro: Kwa hiyo basi, Watu wa Lupo (Luo) na Wahaya na Wanganda hapo kale kutokana kuwa na mzizi wa undugu wa mtoto wa mjumba na mtoto wa shangazi kwa asili walichangia baadhi ya mila na tamaduni kama vile kutopasha tohara watoto wao wa kiume na wa kike.
[1/7, 9:12 AM] Rev.Prof.Ketaro: Na hii ndiyo maana hadi leo hii kuna utani wa jadi ambapo Wahaya huwaita Wakurya kuwa wajukuu zao kwa kuwa chimbuko la Wabantu wa Koo ya Wakurya wote ni Monto bina Sheba bin Raama bin Kushi.
[1/7, 9:15 AM] Rev.Prof.Ketaro: Mfalme Sheba kwa Wabantu wa koo ya Wakurya alikuwa ni babu kwao, wakati kwa Wabantu wa koo ya Wahaya Mfalme huyo alikuwa ni mjomba kwao. Kwa sababu hiyo Mkurya akawa mjukuu kwa Mhaya hadi leo hii.
إرسال تعليق