Rozela ni mmea wenye virutubisho vingi kama vitamini, na madini ya chumvichumvi.

Mmea huu hutumika kwa matumizi yafuatayo:
Hutumika kutengenezea juisi, jam, jellies, sauces, na mvinyo (pombe).
Hutumika kuukinga mwili na magonjwa kama saratani, ini na ukosefu wa lishe.
Unapunguza rehamu, unatibu presha.
Mmea wa Rozela wenye maua mekundu hujulikana kama choya-Dodoma.
Huitwa mkakaka(pwani) na wengine huutumia kama kiungo cha mboga(ndimu).
Majani yake yanaweza kuliwa kama mboga vilevile.
Ni zao la biashara na hutumiwa nyumbani Mrozela.
Mmea huu hukua na hufikia urefu wa mita 3.5 kwa msimu.
Mti pamoja na matawi yake vimenyooka • Majani yamepishana kimpangilio na kugawanyika katika sehemu 3 – 7 pembeni yakiwa kama msumeno.
Una rangi ya kijani, nyeusi hadi nyekundu.
Maua ni makubwa yenye rangi nyekundu hadi njano.
Una mzizi mrefu na hutoa maua wakati wa kiangazi.
Pia unavumilia ardhi yenye tindikali ya juu na ya chini pamoja na magonjwa.

Aina  za  rozela
Kuna aina 2  za Rozela
Hibiscus sabdariffa yenye vikonyo vya rangi nyekundu hadi njano ambavyo vinaliwa.
Hibiscus altissima Webster ambayo hupandwa zaidi kwa ajili ya kamba kamba (fibres) zake lakini vikonyo haviliwi.

Mahitaji ya Mrozela
Hali ya Hewa:
Maeneo ya tropiki yenye mvua kati ya 1500 – 2000 mm kwa mwaka.
Mwinuko wa hadi meta 600 kutoka usawa wa bahari.
Inavumilia joto na hali ya unyevunyevu.
Hupendelea udongo wa mchanga wenye rutuba ambao hupenyeka kwa urahisi.
Hata hivyo unaweza kukua kwenye aina mbalimbali za udongo.
Huhitaji palizi ya mara kwa mara ili kuondoa kivuli na majani.
Huvumilia mafuriko, upepo mkali na maji yaliyotuama.

Ulimaji wa Rozela
Uchaguzi wa eneo, utayarishaji wa eneo, uchaguzi wa mbegu
Mahitaji ya bustani : vikapu, mbolea, udongo, mchanga.
Tifua ardhi vizuri kwenda chini kama sentimeta 20.
Piga mashimo ya ukubwa wa sm15 X sm 15 na kina cha sm 5.
Panda mbegu kilo 11 – 22 kwa hekta.
Ni vyema kupanda mbegu kwa mistari.
Palizi katika mwezi wa kwanza ni muhimu sana.
Mbolea za asili zinafaa kutumika na husaidia sana.
Mtindo wa kubadilisha mazao (crop rotation) hutumika hasa kwa ajili ya mdudu anayeshambulia mmea huu kwenye mizizi (root knot nematode) Heleredera radicicola.
Unaweza kubadilisha na mazao ya kijani kama kunde, mahindi.
Mashamba madogo nyumbani: – Panda mistari halafu ikisha ota punguza iwe katika mistari ya meta 1 x meta 1.

Mashamba makubwa: – Mbegu zioteshwe kwenye kitalu halafu zipandwe shambani kwa upana wa meta1.3 hadi 2.6 na mistari ya upana wa meta 2-3.3 Magonjwa • Fungi: fangas (ukungu) mbalimbali hushambulia kwenye mizizi na majani – Nyunyiza dawa, fungicides Kumbuka: Uangalizi wa shamba unahusisha; – Palizi, Kukata mapukutu, kufyeka – Kunyweshea – Uwekaji mbolea – Uwekaji dawa kwa wadudu waharibifu

Uvunaji wa Rozela
Uvunaji wa matunda na vikonyo hufanyika majuma 3 baada ya maua kuchipua.
Inashauriwa vikonyo viondolewe baada ya kupika matunda.
Kwa Rozela ya kamba: kupanda hadi kuvuna ni miezi 3-4 na ivunwe wakati mimea inatoa maua.
Mimea ikatwe chini kabisa na kisha kuning’iniza ili kamba ziachane na mti – Kamba zioshwe na kuanikwa juani – Mashine zipo na zinaweza kutumika kwa ajili ya kutenganisha kamba na mti.
Ukaushaji Unafanywa kwa kutumia – solar dryer – chekecheke – Kuanika moja kwa moja juani – Kutumia majamvi kwa kukaushia matunda yenye mbegu

Maandalizi.
Andaa turubai, jamvi, mkeka nk.
Bandua vikonyo.
Hifadhi matunda yenye mbegu Kuhifadhi.
Weka rosela iliyokauka kweye mifuko safi ya nailoni au viroba.
Hifadhi mifuko kwenye chumba kisafi chenye mzunguko mzuri wa hewa na kisiwe chenye unyevunyevu

Uvunaji wa kiuchumi
Uvunaji wa vikonyo kilo 1.5-7.5 kwa mmea.
Kilo 17000-19000 kwa hekta.
Uzalishaji wa kamba ni kg 1700 – 3500 kwa hekta
Kiasi cha kamba kwenye rosela ni 5%
Matumizi ya Rozela – Majani, matunda, maua, vikonyo, mbegu, mizizi
Vikonyo vya matunda hutumika kutengenezea jams, jellies, sauces na mvinyo.
Vikonyo pia hutumika kuweka rangi na ladha kwenye vyakula.
Majani machanga huliwa kama mboga.
Mbegu hutumika kwa ajili ya kuongeza nguvu za kiume
Matunda yake yanaliwa.
Kamba zake hutengenezea vitu mbali mbali.
Rozela pia hutoa mafuta.
Inatumika kutengeneza mvinyo mzuri  sana.

Matumizi Ya  Rozela kama dawa asilia
Huongeza nguvu za kiume.
Hutibu magonjwa ya tumbo, majipu, matatizo ya moyo, kikohozi, kansa (vikonyo), homa homa, na magonjwa ya akili.
Hupunguza kiwango cha kulewa kwa mtu anapokunywa pombe.
Maua yake ni mazuri sana katika kupunguza lehemu ( Kolestrol ) kwenye damu.

Rozela  ni zao lenye matumizi mengi yenye faida licha  ya kutumika kama chakula, lakini pia linaweza  kutumika kama  zao la biashara  na hivyo kutengeneza  nafasi nyingi  za ajira.  Ewe kijana mjasiriamali, una ngoja nini ? Anza sasa, lima Rozela,upate kubadilishe maisha yako.

Post a Comment

أحدث أقدم

ZAIDI