Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akipokea maelezo ya namna mashine
zinavyochakata mifuko chakavu na kuzalisha mipya kutoka kwa mmiliki wa
Kiwanda cha SAMAKI Investment ltd Bw. Xiaowei Yu kilichopo Bagamoyo mkoa
wa Pwani, wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani humo Januari 16, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia uzi unaotumika
kutengeneza mifuko maarufu kwa jina la viroba inayozalishwa katika
kiwanda cha SAMAKI kilichopo Bagamoyo mkoa wa Pwani, kulia kwake ni
Katibu Tawala wa Wilaya ya hiyo Bi. Kasilda Mgeni na kushoto ni mmiliki
wa Kiwanda hicho Bw. Xiaowei Yu.
Katibu Tawala wa Wilaya ya
Bagamoyo Bi. Kasilda Mgeni akizungumza neno wakati wa mapokezi ya ziara
ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki
aipotembelea katika kiwanda cha kuchakata mifuko chakavu kilichopo
Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Mmiliki wa kiwanda cha kutengeneza
mifuko cha SAMAKI Bw. Xiawei Yu akieleza jambo kwa ya Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki kuhusu kiwanda
chake alipotembelea kujionea utendaji wa kiwanda hicho Januari 16, 2020.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki akiangalia
namna mifuko ya kubebea bidhaa aina ya (viroba) inavyotengenezwa katika
kiwanda cha SAMAKI ltd kilichopo Wilaya ya Bangamoyo mkoa wa Pwani
alipotembelea kiwandani hapo ili kujionea na kuzungumza na wawekezaji
nchini.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri wa
Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki pamoja
watendaji wa Serikali alioongozana nao katika ziara yake, Mbunge wa
Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete (mwenye t-shit ya kijani) wakiangalia
namna mifuko aina ya viroba inavyotengenezwa katika kiwanda cha SAMAKI
Investment kilichopo Bagamoyo mkoa wa Pwani. Kushoto mwenye tishiti
nyekundu ni mmiliki wa kiwanda hicho Bw. Xiawei Yu.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki pamoja na Katibu Tawala wa Wilaya
ya Bagamoyo Bi. Kasilda Mgeni wakimsilikiza mmlikiki wa kiwanda cha
kuchakata mifuko chakavu cha SAMAKI Investment Bw. Xiawei Yu
walipotembelea kiwandani hapo Januari 16, 2020.
Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani
Kikwete akiuliza jambo kuhusu uzalishaji wa mifuko kwa mmiliki wa
kiwanda cha kuchakata mifuko chakavu cha SAMAKI Bw. Xiawei Yu wa kwanza
kushoto wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
(Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki walipotembelea kiwandani hapo kuona
mazingira ya uzalishaji pamoja na kuzungumza na wawekezaji hao.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri
Mkuu anayeshughulikia maasuala ya Uwekezaji Mhe Angellah Kairuki
akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara yake
katika kiwanda cha kuchakata mifuko chakavu na kuzalisha mipya cha
SAMAKI Investment kilichopo Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia maasuala ya Uwekezaji Mhe Angellah
Kairuki akiwa katika picha ya pamoja na watendaji wa Serikali pamoja na
wafanyakazi wa kiwanda cha kutengeneneza mifuko cha SAMAKI Investment
kilichopo Bagamoyo Mkoa wa Pwani.Kushoto ni Katibu Tawala wa Wilaya ya
Bagamoyo Bi. Kasilda Mgeni, wa tatu kutoka kulia ni Mbunge wa Chalinze
Mhe. Ridhiwani Kikwete.
(PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU)
………………….
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji nchini Mhe.
Angellah Kairuki ametembelea kiwanda cha kuchakata mifuko chakavu na
kuzalisha mipya cha SAMAKI investment ili kukagua mazingira ya
wawekezaji nchini pamoja na kusikiliza changamoto zao na kuzitafutia
ufumbuzi ili kuendelea kuwa na mazingira rafiki kwa wawekezaji nchini.
Waziri huyo
ametembelea kiwanda hicho kilichopo katika Kata ya Zinga Wilaya ya
Bagamoyo mkoa wa Pwani Januari 16, 2020 ili kujionea mazingira yao
pamoja na kupokea changamoto wanazokabiliana nazo ili kuona namna ya
kushirikiana nao katika kuzitatua ili kufikia malengo.
Katika ziara
hiyo aliambatana na viongozi wa Wilaya ya Bagamoyo, Mbunge wa Chalinze
Mhe. Ridhiwani Kikwete pamoja na watendaji wa Ofisi yake ambapo
alifurahishwa na utendaji kazi wa kiwanda hicho kwa kuchakata mifuko
chakavu na kuzalisha mipya pamoja na mifuko ya kisasa na kusema kuwa ni
ya kuridhisha.
“Niwapongeze
sana kwa kuendelea kuzalisha mifuko katika ukubwa tofauti, ikiwemo ile
ya Kilo 25, 50 na 100 na hii itasaidia kuwafikia wateja wenye mahitaji
tofauti tofauti kwa kuzingatia ubora unaotakiwa,” alisema Waziri Kairuki
Alisema licha
ya kazi nzuri inayoendelea katika kiwanda hicho bado kuna kazi kubwa ya
kuwajengea uwezo vijana wa Kitanzania kwa kuhakikisha wanapewa mafunzo
na ujuzi wa kutosha ili waweze kuleta tija katika nchi yao.
Aidha waziri
aliwataka waendelee kuzalisha kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizopo
nchini ili kuendelea kuwekeza kwa uhuru bila uvunjifu wa sheria za
uwekezaji zilizopo.
Aidha akijibu
changamoto zilizoainishwa ikiwemo ya kukosekana kwa huduma za umeme wa
uhakika, ucheleweshwaji wa vibali vya wafanyakazi, kukosa kibali cha
kuingiza malighafi kutoka nchi za nje na ufinyu wa eneo la kiwanda,
Waziri alieleza Serikali itahakikisha inaboresha mazingira kwa
kuhakikisha changamoto za umeme zinatatuliwa na kumwagiza Mhandisi Mkuu
wa Mkoa TANESCO, Kenneth Boymanda kuhakikisha changamoto hiyo
inatatuliwa ifikapo Machi, 2020.
“Nimetembelea
viwanda vingi mkoa wa Pwani na vingi vimeongelea changamoto hii ya
ukosefu wa umeme wa uhakika, hivyo Mhandishi mkuu wa mkoa, hakikisheni
mnamaliza changamoto hii mapema ili kutowakwamisha wawekezaji wetu kwa
kukosa umeme wa uhakika,”alisema Waziri Kairuki.
Naye Mmiliki
wa kiwanda hicho Bw. Xiawei Yu alimshukuru waziri kwa kutembelea
kiwandani hapo na kuahidi kuendelea kuzalisha kwa kuzingatia sheria kama
zinavyoelekeza kwa kuzingatia mradi huo ni mkubwa na una tija kwa jamii
yote kwa kuzingatia umuhimu wa mifuko ya kisasa.
“Tutaendelea
kuzingatia taratibu zilizopo na kampuni yetu imedhamiria kuzalisha
mifuko bora ya kubebea nafaka mbalimbali na kuhakikisha wateja wanapata
bidhaa bora zenye uhakika,”alieleza Bw. Yu.
Aliongezea
kuwa, uwepo wa kiwanda hicho umechangia upatikanaji wa ajira kwa vijana
wapatao 126 kati yao 71 ni wenye ajira rasmi na 55 ni vibarua kwa kazi
ndogondogo za msimu zinazojitokeza kiwandani hapa.
Kiwanda cha
SAMAKI Investment kilisajiliwa tarehe 28 Septemba 2012 na kuanza kufanya
kazi rasmi mwezi Juni, 2013 katika eneo la Mabibo Sokoni eneo la
Urafiki Jijini Dar es Salaam, mnamo mwaka 2017 kutokana na ufinyu wa
eneo, kiwanda kilihamia katika Kata ya Zinga Wilaya ya Bagamoyo mkoa wa
Pwani. Mradi umegharimu wastani wa Tshs bilioni 4. 950 kwa ajili ya
ujenzi na ununuzi wa mitambo ya kisasa kwa ajili ya uzalishaji.
إرسال تعليق