RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amefunga rasmi Maonesho ya Nne ya wiki ya Viwanda ya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) huku akitumia nafasi hiyo kueleza kuna kila sababu ya kuifanya lugha ya Kiswahili iwe ya kuwaunganisha wanachama wa jumuiya hiyo.

Akizungumza baada ya kutembelea mabanda yaliyoko kwenye maonesho hayo pamoja na kuelezea kufurahishwa na namna ambavyo yamefana ametumia nafasi hiyo kuelezea umuhimu wa nchi za jumuiya hiyo kuendelea kusaidiana na kujengeana uwezo ili kuhakikisha wanafikia malengo ya maendeleo na hasa kupitia viwanda.

“Tunaweza kuongeza masoko na ajira kwa kupenda vya kwetu ambavyo vinazalishwa kwenye nchi za jumuiya yetu na ukweli ni chako ni chako na cha mwenzio sio chako. Hivyo umefika wakati wa kupenda bidhaa ambazo zinazalishwa na nchi wanachama wa jumuiya hiyo,”amesema Rais Shein.

Pia ametumia nafasi hiyo kueleza kuna kila sababu ya kuongeza ubora wa bidhaa ili kuvutia wanunuzi wengi zaidi na hiyo itaongeza upatikanaji wa soko la uhakika huku akisisitiza umuhimu wa nchi za SADC ni kuendelea kusaidiana kuendeleza ujuzi na maarifa na hatime kupiga hatua zaidi.

“Maonesho haya yamefana sana na nilitamani kuendelea kutembelea kila banda lakini kutokana na ratiba kubana nimelazimika kutembea kwa baadhi ya mabanda lakini ukweli washiriki wan chi zote wamejitahidi sana na muitikio ni mkubwa.Hata hivyo umefika wakati wa kutumia  Kiswahili kama kiunganishi cha mawasiliano kwa nchi za SADC, najua wapo watakaosema nakipigia debe Kiswahili lakini ukweli uliopo Kiswahili kilitumika kuwaunganisha wananchi wakati wa kukomboa nchi zetu,”amesema.

Pia amesema wananchi waliobahatika kuona maonesho hayo au waliopata taarifa kupitia vyombo vya habari anaamini kuna ujuzi ambao watakuwa wameupata na hivyo kuongeza tija ya uzalishaji wa bidhaa bora.

Hata hivyo amepata taarifa ya uwepo wa mijadala mbalimbali na kushauri mijadala hiyo itumike kutatua changamoto zilizoibuliwa ili kusonga mbele.

“Kulikuwa na mijadala ambayo ililenga kuendeleza na kuweka mikakati kuhusu kuendeleza viwanda katika nchi za SADC na kupitia mijadala hiyo naamini kuna changamoto zimeibuliwa na zimepatiwa ufumbuzi na siku hizi changamoto ni nyingi lakini kuna kila sababu ya kukabiliana nazo,”amesema.

Pia amesema ni vema mijadala hiyo ikaendelezwa kwa njia mbalimbali kwani inatoa fursa ya kupata suluhisho ya changamoto zilizopo hivyo zipatiwe ufumbuzi.

Wakati huo huo amesema Serikali zote mbili za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Zanzibar zinaendelea na mikakati ya kujenga misingi imara katika sekta ya viwanda na biashara pamoja na kutekeleza miradi mikubwa ya kimkakati.

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkurugenzi wa Bishara ya Shirika la Air Tanzania Ndg. Patrick .W.Ndekama, alipokuywac akitembelea banda la maonesho la Air Tanzania katika viwanja vya Ukumbi wa Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakati wa ufungaji wa maonesho hayo(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk. Ali Mohamed Shein akimsikiliza Afisa wa TRC Bi. Jamila Mbarouk alipotembelea banda la maonesho katika viwanja vya Kulius Nyerere Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk.Ali Mohamed Shein, akimsikiliza Afisa wa ZSTC Ndg. Issa Hamad Ramadhani alipotembelea maonesho ya Wiki ya Nne ya Viwanda ya SADC Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)

 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akiwa na Viongozi wa Serikali na SADC WAakiwa wamesimama wakati ukipigwa Wimbo.(Picha na Ikulu)

 KATIBU Mkuu wa SADC Mhe. Dr.Stergomena Tax, wakati wa ufungajin wa Maonesho ya Nne ya Wiki ya Maonesho ya Viwanda ya SADC leo Jijini Dar es Salaam.yaliofanyika katika ukumbi wa Juluis Nyerere.(Picha na Ikulu)
KAIMU Waziri wa Biashara na Viwanda Zanzibar Mhe. Mahmoud Thabit Kombe akizungumza wakati wa mkutano wa Ufungaji wa Wiki ya Nne ya Maonesho ya Viwanda ya SADC Jijini Dares Salaam.(Picha na Ikulu)
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza kwenye Ukumbi  wa Mikutano wa Kimataifa wa  Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam wakati akifunga  Maonesho ya Nne ya wiki ya viwanda kwa Jumuiya ya maendeleo kwa nchi za Kusini mwa Afrika(SADC) 
 Viongozi mbalimbali wakiwa mezaa kuu wakifuatilia kwa makini hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)wakati anafunga maonesho ya wiki ya nne ya viwanda kwa nchi za SADC yaliyofanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam .
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza wakati akifunga maonesho ya nne ya wiki ya viwanda yaliyokuwa yakifanyika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalim Nyerere jijini Dar es Salaam pamoja na viwanja  vya Karimjee jijini.

Post a Comment

أحدث أقدم

ZAIDI