Tarime. Walimu 16 wa Shule ya Msingi Kenyamanyori halmashauri ya mji wa Tarime mkoani Mara wamekamatwa na polisi kwa madai ya kumruhusu anayedaiwa kutokuwa mwanafunzi kufanya mtihani wa kuhitimu darasa la saba.



Walimu hao waliopangiwa kusimamia mitihani katika shule mbalimbali, walijikuta wakitakiwa kukabidhi bahasha za mitihani na fedha walizopewa kwa ajili ya kusimamia kisha kurejea kwenye vituo vyao vya kazi.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Septemba 12, 2019 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa amesema, “Ni kweli tukio hilo lipo, wamekamatwa inaonekana kuna namna na walishirikiana.”

Chanzo cha taarifa hizo kinaeleza kuwa walimu hao walibainika baada ya taarifa kutumwa ofisi za elimu Mkoa wa Mara kuwa kuna mwanafunzi feki miongoni mwa  wanaofanya mtihani huo ulioanza jana na kumalizika leo.

Post a Comment

أحدث أقدم