Je, unapenda kufungua mitandao mbalimbali ya jamii kama Facebook, Tweeter, Instagram, Google Plus, Snapchat, LinkedIn, Youtube na mingineyo kila siku?
Kama jibu ni ndiyo, basi uko hatarini kupata tatizo la msongo wa mawazo na wasiwasi.
Utafiti mpya uliofanywa na Chuo Kikuu cha Pittsburgh cha Pennsylvania nchini Marekani mwaka 2014 na kuzinduliwa mwaka huu, unaonyesha kuwa matumizi ya mara kwa mara ya mitandao ya jamii yanaweza kusababisha magonjwa ya akili, ukiwamo msongo wa mawazo na wasiwasi.
Wakati kukiwa na tatizo hilo, inakadiriwa kuwa asilimia 71 ya vijana duniani kote hutembelea mitandao tofauti ya jamii kila siku huku simu za mikononi zinazowezesha kupatikana mitandao hiyo kirahisi zikizidi kubuniwa na kuboreshwa.
إرسال تعليق