Inapofika mahali umemchoka mpenzi wako ni bora umwambie kwa maneno
matupu tena ya bila kupindisha kwamba nimekuchoka sikutaki tena sitaki
mahusiano na wewe tena nenda zako, ukieleza kifupi hivyo utaeleweka
vizuri tu na kama huyo unaemwambia ana akili timamu wala hawezi
kuendelea tena na mahusiano na wewe au kukulilia kama vile wewe ni mungu
kwake ikiwa umemtamkia maneno mazito kama hayo.
Lakini tabia ya kuachana kwa maneno mazito yenye matusi mazito mazito
yanayohusisha mpaka na wazazi na ndugu wengine ambao hawayajui hata
mahusiano yenu tabia hii huwa sio nzuri kabisa, kwanza inaonyesha
hujakua hata kidogo na akili yako finyu na ndogo kama tonge la ugali wa
mtama.
Mwanamke au mwanaume aliekuwa ki akili cha kwanza ni lazima kinywa chake kiumbwe na maneno ya busara, hekima na adabu, no matter how/haijalishi mmeudhiana vipi katika mahusiano na mmefikia stage ya kuachana ni lazima muachane kwa busara, tabia ya kukamuliana matusi kama chunisi dume au ndimu kwenye samaki kukata shombo inaprove kwamba wewe ni zero brain kiasi gani katika maisha yako.

إرسال تعليق