Kumekuwa na tabia au hali ya wanawake wengi kupiga kelele au unaweza
kusema kutoa sauti wakati wakishiriki tendo la ndoa. Hali hii imeacha
maswali kama kutoa huko sauti ni jambo la asili au ni mwanamke mwenyewe
anaamua hapa atoe sauti na kwingine asitoe.
Mwaka 2011 watafiti wawili mmoja kutoka Chuo Kikuu cha Lancashire na
mwingine kutoka Chuo Kikuu cha Leeds wote wa nchini Uingereza
walichapisha utafiti wao walioufanya uliokuwa ukihusu utoaji wa sauti wa
kati wa kujamiina. Walitaka hasa kujua kwanini wanawake hutoa sauti
hizo.
Katika utafiti huo, waliwahoji wanawake 71 wenye umri kati ya miaka 18
na 48 ambao hushiriki mapenzi mara kwa mara juu ya utoaji wa sauti
wakati wa kujamiiana.
Katika utafiti huo ulibaini kuwa wanawake wengi huto sauti hizo lakini
sio pale tu wanapokuwa wamefika kileleni. Asilimia 66 walisema kuwa
hutoa sauti wakati wa kujamiina ili kuwasaidia wenza wao kufika
kileleni haraka, wakati asilimia 87 walisema kuwa hutoa sauti hizo ili
kuwaongezea wenza wao kujiamini kwa kile wanachokifanya kuwa wapo sawa.
Wanawake walieleza kuwa mara nyingi hutoa sauti wakati wenza wao
wanapofika kileleni. Baadhi pia walieleza kuwa sauti hizo huwasaidia
kuwaondolea uoga walionao, hali ya kutojisikia kuwa sawa, wakati
mwingine kuondoa maumivu lakini pia kama njia ya kufurahia raha
anayokuwa anaipata.
Aidha, wataalamu hao walisema kuwa kwa vile wanaume wengi huhusisha
utoaji wa sauti na mwanamke kufika kileleni, basi baadhi ya wanawake
hutoa sauti hizo kwa uongo ili tu kuwaridhisha wenza wao waone kila kitu
kipo sawa.
Kwa upande mwingine, imegundulika kuwa wanawake si jamii ya wanyama
pekee ambao hutoa sauti wakati wa kujamiiana kwani hata nyani (baboons)
wana aina zao za sauti ambazo huzitoa wakati wakijamiiana.
Imeelezwa kuwa wakati mwingine huwa ni vigumu sana kuelezea kila
kinachotokea wakati wa kijamiiana kwa sababu kila mtu huwa na utashi
wake. Lakini kitu wataalamu walichokubaliana ni kuwa sauti hizo zinaweza
kumsaidia mwenza kujua kama anachofanya ni sasa hivyo aendelee au
aache, aongeze au apunguze.
Andika Maoni yako Hapo Chini Utuambie nini Kinamfanya Mpenzi Wako Apige
Kelele Wakati wa Kuhondomola au Kama Wewe ni Mwanamke Tueleze Sababu ya
Nini Kinapelekea Hadi mnapiga kelele wakati wa game,Zingatia Lugha yenye
tafsida isiyokuwa na matusi.
إرسال تعليق