Afrika ni bara la pili Duniani kwa ukubwa likiwa na eneo la kilomita za mraba 30,244,050. Lakini Asia ndio bara pekee kubwa kushinda Afrika.

Neno “Afrika” limetokana na lugha ya kilatini ya waroma wa kale. Waroma kwa jina hilo hawakumaanisha bara lote bali ni eneo katika nchi ya Tunisia ya leo tu, Asili yake ni kabila la Afrig lililoishi sehemu zile.

Wakati huo Wagiriki wa kale walitumia zaidi jina la Libya kwa ajili ya nchi za kusini ya bahari ya Mediteraneo. Maeneo ya ndani kuelekea kusini mara nyingi yalijulikana kwa jina la Ethopia linalomaanisha nchi ya watu weusi (Kwa kigiriki aithiops aliyechomwa na jua).

Sasa hapa tufahamishane zaidi juu ya bara letu hili…..Karibu!

Idadi ya nchi zipatikanazo barani Afrika ni 54, huku Sudan Kusini ikiongezeka hivi karibuni na kuwa nchi moja wapo ya Afrika mwaka 2011, mwezi wa 7, tarehe 9.

Na kuhusu mlima mrefu barani Afrika ni Mlima Kilimanjaro, ambao unapatikana nchini Tanzania na una urefu wa mita 5895.

Jangwa kubwa barani Afrika ni jangwa la Sahara lenye ukubwa wa kilomita za mraba 9,000,000, na limeenea hasa Afrika ya Kaskazini.

Mto mrefu barani Afrika ni Mto Nile ambao pia ni mto mrefu duniani ambao chimbuko lake ni pale katika Ziwa Victoria na kuelekea hadi nchi ya Misri urefu ni kilomita 6650

Ziwa kubwa Afrka ni Ziwa Victoria, ambalo lipo katika nchi za Tanzania, Kenya, na Uganda. Ziwa Victoria pia ni la pili kwa ukubwa duniani lenye ukubwa wa kilomita za mraba 68,800. Pia ni chanzo kikuu cha mto Nile.

Kisiwa kikubwa barani Afrika ni Kisiwa cha Madagascar kipatikanacho katika pwani ya bahari ya Hindi Afrika Mashariki. Pia ni kisiwa cha nne kwa ukubwa Duniani, Kisiwa cha Madagascar kina urefu wa kilomita 1580 na upana wa kilomita 570.

Nchi yenye wakazi/ wanachi wengi barani Afrika ni Nigeria ambayo inawakazi wanakadiriwa kufika kati ya watu million 125 hadi watu 145 million. Huku ikifuatiwa na nchi ya Misri yenye wakazi wapatao million 76.

Nchi yenye wakazi wachahe barani Afrika ni nchi ya Shelisheli inawakazi wapatao 80,000 .

Mji wenye wakazi wengi barani Afrika ni mji wa Cairo wa Misri wenye wakazi wapatao million 17 na mji wenye wakazi wachache barani Afrka ni Maseru unaopatikana katika falme za Lesotho na una idadi ya watu karibu 14,000.

Idadi ya Makabila yapatikanayo barani Afrika inaamimika kufika makabila 3,000, ambapo nchi kama Nigeria peke yake ina makabila yapatayo 370.

Idadi ya Lugha zinazozungumzwa barani Afrika ni Lugha Zaidi ya 2,000, huku kiarabu kikiwa kinazungumzwa sana kwani takribani ya watu million 170 wengi wao wanazungumza kiarabu.

Bara la Afrika lina takribani miji mikuu 54.

Nchi ambazo wageni hupenda kutembelea katika Afrika Mashariki ni Tanzania na Kenya kwani nchi zote hizo mbili zinavivutio mbalimbali ambavyo huwavutia wageni ikiwa ni pamoja na masuala ya safari za kutembelea hifadhi za wanyama pori na kupumzika katika fukwe za bahari ya Hindi.

Nchi ambazo wageni hupenda kutembelea katika Kusini mwa Afrika ni nchi ya Afrika Kusini, ambayo ni nchi maarufu zaidi, wageni huvutiwa na miji ipatikanayo, fukwe, hifadhi za wanyama pori, pamoja na utalii wa matibabu.

Nchi ambazo wageni hupenda kutembelia katika Afrika Magaharibi ni Gambia na Senegal, kwani huwavutia watalii kwa umaarufu wa fukwe zenye unafuu kwa watalii waliokimbia hali ya hewa ya baridi baridi.

Nchi ambayo wageni hupenda kutembelea katika Afrika ya Kaskazini ni Misri, ambayo ni kivutio kwa utalii, pia pamoja na nchi kama Morocco na Tunisia.

Nchi zinaongoza kwakutembelewa sana na watalii barani Afrika ni Misri, ambapo mnamo mwaka 2007 iliwezakupokea watalii wapatao takribani million 10, huku Afrika Kusini ikiwa ni nchi ya pili kwa kuwa ni sehemu ambayo huwavutia sana wageni na kwenda kutembelea ambayo ilipokea wageni takribani million 9 kwa mwaka 2007, takwimu hizo ni kwa mujibu wa (UNWTO

Post a Comment

أحدث أقدم

ZAIDI