•  
Waathiriwa wa kirusi cha corona nchini Kenya wamefikia watu saba baada ya watu wengine watatu kuthibitishwa kuambukizwa kirusi hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano, Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema kuwa, watu wote hao saba wametoka nje ya Kenya. Wawili kati ya wagonjwa hao watatu wa karibuni kabisa wametokea Madrid Uhispania kupitia Dubai na mgonjwa wa tatu ni raia wa Burundi aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi akitokea Dubai pia.
Huku hayo yakiripotiwa, Wizara ya Afya ya Afrika Kusini imetangaza kuongezeka idadi ya waathiriwa wa kirusi cha corona nchini humo na kufikia watu 85 ikiwa ni ongezeko la watu 34 ikilinganishwa na taarifa ya kabla yake.
Kabla ya hapo Wizara ya Afya ya Afrika Kusini ilikuwa imetangaza kuwa watu 51 wameambukizwa kirusi cha corona nchini humo.

Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini

Katika juhudi za kupambana na maambukizi ya kirusi hicho hatari, viongozi wa Afrika Kusini wameziweka chini ya karantini meli mbili karibu na Capetown,  moja ni meli ya mizigo na nyingine ni ya kitalii.
Meli ya kitalii kati ya hizo mbili ina abiria elfu moja na 240 na wahudumu 486.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini ametangaza hali ya "Janga la Taifa" katika maeneo yote ya nchi hiyo kufuatia kuenea kwa kasi maambukizi ya kirusi cha corona, ugonjwa ambao jina lake rasmi na COVID-19.

Post a Comment

أحدث أقدم