“Kafanyeni kazi na mkaridhike na mlichonacho, shida kubwa ya Vijana wengine ukiwapa nafasi wana shida ya kutoridhika na nafasi walizonazo, bila kuelewa kuna miaka mingi, nitamshangaa leo IGP akienda Bunda akaenda kugombea akitegemea nitamteua kuwa Waziri” -JPM

“Nitakushangaa RC Morogoro uwe una mpango wa kwenda Monduli kugombea Ubunge, nitamshangaa CDF akienda kugombea ili awe Waziri wa Ulinzi, nitamshangaa IGP akigombea Ubunge, kwanza unaweza kugombea nikakutata jina lako vilevile, tukamchukua mshindi wa 3, itategemea nimeamkaje”-JPM

“Natoa wito kwa Viongozi ninaowateua kujifunza kuridhika na nafasi walizonazo, huwezi ukawa na kila kitu, lakini Demokrasia iko huru siwazuii kwenda kugombea kama unaamua kwenda kugombea uongozi nenda tu”-JPM

Post a Comment

Previous Post Next Post