Katika
hali isiyotarajiwa, Ann Magwi na Jonathan Munini, kutoka Tana River
Kenya, wamelazimika kukatisha zoezi la kufunga ndoa, baada ya James
Sidai kujitokeza kanisani na kusema yeye ndio Baba yao Mzazi.
Baba huyo aliingia kanisani akiwa na Dada yake na kusema ndoa hiyo isifungwe kwa kuwa Maharusi ni Ndugu wa damu.
“Mama
zenu nyie, mmoja aliniacha akaondoka na mtoto akiwa na mwaka mmoja,
mwingine aliona uchumi wangu umeyumba akaondoka akiwa na mimba ya miezi
minne na akaolewa na mwalimu, nikaamua kumuoa mwingine na tuna watoto
watatu, nimeona tangazo la harusi yenu WhatsApp zile picha nikasema hawa
ni wanangu nikachunguza kwa watu mlioishi nao wakasema ni kweli,”
James.
Bwana
harusi ambaye ni mfanyabiashara katika mji wa Madogo aliondoka kanisani
kwa hasira akimuacha mama yake akiwa analia huku bibi harusi akiondoka
na mama yake ambaye inadaiwa alikuwa amepoteza fahamu.
إرسال تعليق