Kuna wanawake wa aina nyingi hapa duniani.Kuna baadhi ya tabia zao zikianza kujionesha katika mahusiano yenu jua kuwa taa nyekundu imeshawaka na yakupasa ushtuke na usepe mapema.


Mwanamke ambae hakusalimii wala kukujulia hali wala kukutakia usiku mwema mpaka umuanze wewe jua kabisa kuwa haupo kwenye moyo wake. Hapa ndugu unatakiwa ushtuke mapema na ikiwezekana temana nae.


Mwanamke ambae ukimtumia sms zako anazisoma halafu hakujibu ontime kwa kisingizio kuwa yupo busy na kazi , na anajibu anavyojisikia yeye labda baada ya siku moja su hata wiki baada ya kuzisoma jua kuwa huna umuhimu kwake ,hivyo inakupasa ujiongeze.

Ahlan wa sahlan


Mwisho ni mwanamke ambae ukiona anakutafuta au kukujulia hali yako ni pale tu anapokuwa amekwama kiuchumi.Huyu temana nae na umfungie vioo kabisa maana hakufai ,umuhimu wake kwako ni katika masuala ya pesa tu.

Post a Comment

أحدث أقدم