Feisal Salum Atuma Salamu Kwa Waajiri Wake wa Zamani Yanga "Watajua Hawajui"


Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah “Fei Toto’, ametuma ujumbe mzito kwa waajiri wake wa zamani Young Africans kuelekea mchezo wao wa Oktoba 25, mwaka huu kwa kuweka wazi amejipanga kuendeleza kasi ya kutupia mabao na kuisaidia timu yake kushinda mchezo huo.

Azam wanaokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zao 13 walizokusanya katika michezo yao mitano ya kwanza ya Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu, Oktoba 25 mwaka buu wanatarajiwa kuwa wageni wa Young Africans kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kupigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es salaam.

Fei Toto aliyejiunga na Azam FC akitokea Young Africans amekuwa kwenye kiwango bora ambapo mpaka sasa anakamata nafasi ya pili katika chati ya wafungaji kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kufunga mabao manne kwenye michezo mitano.

Fei Toto amesema wanapambana kusaidia timu yake kufikia malengo kuhakikisha inapata ushindi katika kila mchezo pamoja na kuona anafikia malengo ya kuwa mfungaji bora wa msimu huu.

“Tuna malengo makubwa msimu huu kama timu, kila mchezaji ana morali ya kuhakikisha anaisaidia timu kupata matokeo mazuri kwa kila mechi kwa sababu tunahitaji kutwaa taji la ubingwa wa ligi.

“Tunafahamu utakuwa mchezo mgumu, lakini kila mchezo kwetu tunaupa umuhimu mkubwa, binafsi matarajio yangu ni kuendelea kufunga kwenye kila mchezo na kuisaidia Azam FC kufikia malengo.”

Post a Comment

Previous Post Next Post