Na Hashim Mbaga 

Simba Sports club Limited Imefanya Press yake kubwa sana chini ya CEO Mr. Magori na kutangaza Rasmi Msimu mpya kuanza kwa mwaka wa 10 mfululizo kwa Tamasha kubwa la Simba Day.

Mwaka huu Simba Day imepata hamasa sana na imepangiliwa kwaa ufasaha kwa kupata vionjo vipya ikiwemo mdhamini Mkuu wake Sportpesa kushirikiana katika kufanikisha Tamasha hili hivyo ikabidi kufanya Joint ya kibiashara ya Jina na kuwa Rasmi ni Sportpesa Simba Week.

CEO Aliweza kutaja Rasmi Matukio kama Ifuatavyo:

31/07/2019 - JUMATANO

WACHEZAJI KUWASILI DSM
Mabingwa wa nchi, Mabingwa wa kihistoria wa Kagame Cup na Wataalam pekee waliofika Quarter final Champions League Caf kwenye Ukanda huu wa Africa Mashariki na Ndio Wafanikishaji wa kihistoria kuweza Tanzania kuingiza Interclub timu 4 wanaingia Toka kwenye Camp yao iliyowekwa Sports Campus iliyoko Kwenye viunga vya Hotel ya kifahari  The Royal Manang 5star jiji Rustenburg nchini South Africa wakitua na Ndege ya wazalendo Air Tanzania.

KUSAINI MKATABA
Kutakuwa na Press Serena Hotel kuanzia Saa 5 Asubuhi katika hafla ya kusaini mkataba kati ya Simba na Romario Sports 2000 kwa ajili ya Vifaa vya michezo na Jezi kwa ujumla pia Faida ya kimkataba baina yao wataweka wazi.

UZINDUZI WA JEZI MPYA
Ifikapo saa 6 usiku Kwenye mitandao rasmi ya Simba yote pamoja na Sponsor wote wa Simba kutawekwa Jezi mpya za msimu huu zitakazotumika za Rangi 3 tofauti Red, White na Gray.
Watu wote muda huo Usikose Angalia uyape macho ladha yake ndani ya moyo wako.....KUNA ANAETASEKA HAPA?

01/08/2019 - ALHAMISI
UUZAJI WA JEZI
Hii ndio siku rasmi Jezi zote zinaanza kuuzwa nchi nzima na zitapatikana maeneo yote makubwa na mikoa yenye mashabiki wa Simba kirahisi.
Kutatangazwa vituo/sehemu za kupatikana Jezi.

KUUZA TIKETI
Mwanzo wa kuuzwa Tiketi za Aina Mbili ambazo ni Platinum na Platium Plus.
Bei ya Tiketi zote  ni kama ifuatavyo:
Mzunguko  5,000
VIP B        15,000
VIP A        30,000
Platinum 100,000
Platinum Plus 150,000

Kifupi Vingezo au huduma zitakazopatikana kwenye Tiketi za Platinum zitatangazwa baadae ila baadhi yake ni
- Kukaa eneo mahsusi uwanjani
- Kupata usafiri mzuri kwenda
- Kupata jezi Original
- Kupata fursa ya Picha na Wachezaji uwatakao siku maalum wwewena familia yako.
- Kupata vinywaji nk nk.

KADI MPYA ZA SIMBA
Kutakuwa na Press kubwa sana Serena Hotel katika Tukio la Karne la kutanganza Card Mpya ya Simba.
Kutakuwa na kusainiana mikataba na Washirika wa kibiashara watakaosaidia katika kazi hiyo ili kuweka ufanisi.
Kutaelezwa kila kitu kuhusu upatikanaji wa card na utumiaji wake.
Card zinazokusudiwa kutolewa ni kwa Wanachama waliopo New Members Card, na wapenzi/mashabiki wa Simba New Fans Card ambazo kwa hawa fans ndio ili uwe mwanachama mpya hapo baadae lazima upitie kwenye eneo hili kwanza.
Kadi zinazotolewa sasa zitakuwa na uwezo wa kuhifadhi fedha, kuingilia uwanjani,  kulipia michango nk, kununulia bidhaa mbalimbali kwa Punguzo maalum kifupi zinaitwa E-CARD.

02/08/2019 - IJUMAA

Ni siku maaalum kwa Simba Sports club kutembelea Sponsor wake wote kwenye vituo/ofisi Zao.
Tunaanzia Sportpesa Saa 3 asubuhi halafu Saa 5 kwenda Azam Media na kuendelea.


03/08/2019 - JUMAMOSI

SPORTPESA STREET VISIT
Kampuni ya Sportpesa ikishirikiana na wachezaji wa Simba itafanya au unatembelea Vituo vya Watoto wenye vipaji maalum na mazingira MAGUMU katika kutoa msaada na hamasa kwa jamii.

OCEAN ROAD HOSPITAL
Wachezaji wote wa Simba watatembelea kutoa Pole, faraja na mkono wa heri kwa wagonjwa wote, wasiojiweza na katika kurudisha Shukrani kwa jamii.

WATU WOTE NCHINI
Tunaomba wote kama kawaida sehemu mbalimbali na matawi yote siku hii wakati wachezaji wanaenda Ocean road Hospital nao popote walipo Waende kwenye Hospital au vituo vya Jamii katika kufanya tukio la kijamii.
Pia Wote Tuweze kutoa Damu kama tunavyofanya kila mwaka kwa DSM Tutatangaza Vituo vitakuwa wapi baada ya kushauriana na wenzetu wa Benki ya Damu nchini.

WIMBO WA SIMBA
Kutatambulishwa Wimbo rasmi maalum wa club yetu ya Simba ambao tutakuwa tunauimba mahali popote kuonyesha ufahari wetu.
Utagusa, utaleta hisia na Ushujaa miongoni mwetu na kisababisha ujasiri wa Upambanaji ndani ya Uwanja na Nje ya Uwanja Lengo kuu ni Nguvu Moja.

04/08/2019 - JUMAPILI
KUPIGA PICHA NA WACHEZAJI
Tukio hili limebatizwa jina linaitwa *Photoshoot With Simba Stars*
Ni tukio ambalo itafanyika Serena Hotel kuanzia saa 4 asubuhi kwa watu wote walikataa Tiketi za Platinum na Platinum Plus kuweza kuja na Family zao hasa watoto ili kupiga picha na Wachezaji wanawao wapenda pamoja na kuandika majina wayapendayo kwenye jezi zao.

Baada ya hapo Wachezaji wote wanakwenda kutembelea Vituo vya Watoto Yatima na Mazingira magumu katika kutoka sadaka kwa niaba ya Club ya Simba.



Mwisho siku hii tutamalizia kwa kuwapokea Timu Marafiki wetu wanaokuja kucheza nasi siku ya kilele cha Sportpesa Simba Week timu ya Power Dynamos ya kutoka Zambia.

05/08/2019 - JUMATATU
SIMBA QUEENS
Wachezaji wote wa Simba Queens na warimbwende wa Simba watatembelea Shule ya Makongo Secondary kwa ajili ya kutoa/kuonyesha/Kuwaasa kwa pamoja jinsi ya kuishi, kucheza, elimu na EXPOSURE kwa ujumla walionayo na walioipata toka Germany.

RATIBA YA KIBABE
Saa 8:30 Mchana - Pre match inayofanyika Uwanja wa Taifa.

Saa 9:30 Mchana Press za timu zote mbili zitafanyika.

Saa 10:30 jioni Simba Watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa

Saa 11:30 jioni Power Dynamos watafanya mazoezi Uwanja wa Taifa.

06/08/2019 - JUMANNE

Hii ndio siku ambayo nchi nzima inatakiwa kuwa Red yote.
Uwezekano wa Kuwekwa Screen kubwa uwanjani sehemu mbalimbali Dsm na mikoani unafanyiwa kazi ili wote wana Simba waweze kuangalia pamoja tukio hili la Simba popote ulipo.

SAA 4 ASUBUHI
Milango yote inakiwa wazi watu waweze kuanza kuingia uwanjani.

SAA 8 MCHANA
Timu ya Simba Queens inacheza ndio itazindua uwanja kwa mechi.

SAA 9 MCHANA
Timu ya Simba U20 itacheza na FontainGate Academy.

SAA 10:30 JIONI
Utambulisho wa mbwembwe wa wachezaji wote wa Simba.

SAA 11:30 JIONI
Ule mchezo rasmi ndio itacheza
Simba vs Power Dynamos.

07/08/2019 - JUMATANO
Kutakuwa na After Sportpesa Simba week Party ni Dinner maalum kwa wageni maalum katika kuwashukuru kufanikisha Sportpesa Simba week wakiwepo Sponsors, Makundi mbalimbali ya Simba, Wachezaji wa Timu zote ppamojana kuwaagaa timu ya Power Dynamos.

SLOGAN YA MWAKA HUU
Mwaka huu kwenye Sportpesa Simba Week tunakwenda na kauli mbinu maalum na ambayo
Tunaomba kila MwanaSimba akipost kitu amalizie na:
IGA UFE: #This is next level#

Post a Comment

أحدث أقدم