Alizeti ni moja kati ya mazao ambayo hupatikana hapa nchini katika baadhi ya mikoa ikiwemo Singida na Iringa. Zao la alizeti hutumika hasa kwa kuchuja mafuta yake ambayo hutumika sana kwa kupikia. Lakini alizeti zinapochunjwa hutoka uchafu, uchafu huu huitwa mashudu, ambayo ni mazuri sana kwa ajili ya mifugo. Kwa wale ambao ni wafugaji wenzangu nadhani hapa watakuwa wanaelewa vizuri nazungumzia nini hasa.
Naomba hapa nikuarike ili uweze kujifunza faida ya mbegu za alizeti kama ifutavyo; mbegu mbichi za alizeti ni tiba ya mishipa ya fahamu. mapafu mafua na kifua.
Alizeti pia zina uwezo mzuri wa kuimarisha mifupa kutokana na kuwa na madini ya ‘magnesium’ na ‘copper’ ambayo husaidia kuifanya mifupa kuwa imara.
Hali kadhalika alizeti zimesheheni vitamin E, ambayo husaidia kuondoa maumivu ya viungo katika mwili pamoja na kupambana ana miale hatari ya jua yaani 'UV rays' na hivyo kumfanya mhusika kuwa na ngozi nzuri muda wote.
Matumizi ya robo kikombe cha alizeti huweza kukuweka mbali zaidi na uwezekano wa kushambuliwa na maradhi ya moyo, kutokana na uwezo wake wa kukabiliana na mafuta hatari mwilini ‘cholesterol’ hivyo kumuepusha mhusika na shambulio la moyo.
Hivyo kila wakati unashauriwa kutumia alizeti kwa faida kem kem.
Post a Comment