Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel ameungana leo na mwenzake wa Ufaransa Emmanuel Macron na viongozi wengine wa Umoja wa Ulaya, akisema kuwa moto unaouteketeza msitu wa mvua wa Amazon unaweka kitisho kwa dunia nzima na unapaswa kujumuishwa kwenye mada za mkutano wa kilele wa kundi la nchi saba tajiri duniani - G7 utakaoanza kesho.

Msemaji wa Merkel, Steffen Seibert amesema Kansela Merkel ameshawishika kuwa suala hilo ni la dharura kubwa na linapaswa kuwekwa kwenye ajenda.

Serikali ya Ufaransa imesema leo kuwa itazuia mpango wa kibiashara kati ya Umoja wa Ulaya na Amerika Kusini kuhusiana na sera za Brazil.

Bolsonaro alimshambulia Macron kwenye mtandao wa Twitter akisema anasikitika kuwa rais huyo wa Ufaransa anataka kutimiza maslahi binafsi ya kisiasa katika suala la ndani la Brazil na nchi nyingine zilizoko katika eneo la msitu wa Amazon.

Post a Comment

Previous Post Next Post