Tume ya Taifa ya Uchaguzi ili kutangazia Umma kuhusu Uchaguzi Mdogo wa Udiwani katika Kata 13 za Tanzania Bara utakaofanyika tarehe 17 Agosti mwaka 2019,kwakuzingatia matakwa ya kifungu cha 13 (3) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa Sura Na. 292.

Kwa mujibu wa ratiba ya uchaguzi huo, Utoaji wa Fomu za wagombe au lipangwa kufanyika kuanzia tarehe 29 Julai hadi 03 Agosti, 2019 na Uteuzi wa wagombea kufanyika tarehe 03 Agosti, 2019.

Hadi kufikia leo tarehe 02 Agosti, 2019 saa 10:00 jioni jumla ya wagombea 60 kutoka vyama vya siasa 18 wamechukua fomu za uteuzi.

Vyama vilivyochukua fomu hadi sasa na idadi ya wagombea walio chukua fomu kwenye mabano ni Chama cha DEMOKRASIA MAKINI(5) AAFP (5), CCK(3), DP (4), SAU (4), UDP(4) ACT Wazalendo (3), UPDP (5), ADC (2), TLP (1), CCM (12), ADA TADEA (4), CHADEMA (2), CHAUMA (1), NRA (1), NLD (1), CUF (2)na UMD (1).

Post a Comment

أحدث أقدم