Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa morogoro  wilbrod mutafungwa,ametoa wito kwa wanachi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi ili taarifa zote zinazohusu viashiria vya uhalifu  vifanyiwe kazi mara moja.

Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari  amesema hali ya mkoa huo ni shwari na hakuna matukio makubwa yanayotishia usalama wa raia na mali zao, amesema bado wanaendelea na jitihada mbalimbali za kukabiliana na matukio ya kiuhalifu na wahalifu.

Mutafungwa amesema katika msimu huu wa sikukuu za krismas na mwaka mpya polisi mkoa wa morogoro wamejipanga vizuri kuhakikisha wananchi wanahudhuria katika nyumba za ibada na kushiriki ibada za kusherehekea siku hizi kwa utulivu na amani.

Hata hivyo, kamanda mutafungwa amesisitiza kuwa kutakuwa na ulinzi wakutosha katika nyumba za ibada, majengo ya serikali, benki, masoko, kumbi za starehe, viwanja vya michezo pamoja na kuimarisha doria katika barabara zote kuu pamoja na barabara za mitaani, kwamba kutakua na doria za masafa marefu, pamoja na doria za miguu na doria zinazoambatana na wanyama wakali (mbwa wa polisi).

Katika hatua nyingine jeshi la polisi limetoa motisha kwa askari wake ambapo walishiriki kuokoa maisha ya baba na motto ambalo limetokea siku chache zilizopita katika maporomoko ya nguzo campsite.

Kwa upande wake diwani wa kihonda khamisi kilongo, ambapo ndio wanapoishi baba huyo na mwanaye amelipongeza jeshi la polisi kwa hatua iliyochukua na kusema ni hatua kubwa katika kuleta hamasa kwa askari katika kufanya vizuri na ameomba hii iwe zoezi endelevu kimkoa na ikiwezekana hata taifa zima.

Onesmo kahemere ni miongoni mwa askari walioshiriki uokoaji ameelezea jinsi hali ilivyokua ambapo amesema kama askari licha ya kuwa alikua akitimiza wajibu wake lakini pia aliguswa kibinaadamu kufanya hivyo.

Post a Comment

Previous Post Next Post