Kwa kawaida Mwanaume unapohitaji kuanza uhusiano na msichana unaempenda
sana, kiu na njaa ya kuwa naye huwa iko katika kiwango kisichopimika.
Hasa unapokuwa unaanza kuwasiliana nae na ukafanikiwa kumsogeza karibu
na kumuonesha kwa vitendo kuwa unampenda na kwa bahati nzuri, akaanza
kukuwashia ‘Taa ya Kijani’.
Hata hivyo, mwanzo huu unaweza kuwa mbaya kwako endapo hautazingatia
kanuni moja muhimu sana kati ya kanuni nyingi za kuendeleza na kudumisha
mapenzi yaliyochipua yanayohitaji mbolea na maji safi kutoka kwako ili
yachanue.
Ingawa ukweli ni kwamba muonekano wake na mvuto alionao mwanamke
unaempenda unaweza kuwa ndio chanzo kikubwa kilichokusukuma kumfuata na
kuanzisha maongezi kwa mara ya kwanza, ni muhimu sana kutomuonesha
dalili zozote kuwa ‘ngono’ ndio hitaji lako la kwanza au kitu ulichokipa
kipaumbele.
Kabla hujamwambia kitu chochote, kumbuka yule ni mtu mzima, mrembo
aliyewavutia wengi kabla yako. Jiulize maswali kadhaa, je, kwa makadirio
ya haraka haraka unadhani kuna neno jipya utakalomwambia ili akuamini
wewe tofauti na wanaume wengine waliowahi kuongoa naye?
Hapo ndipo utagundua kuwa maneno yako yana nafasi ndogo sana kwake hivyo
unapaswa kuyachagua kwa umakini mkubwa ili yapenye masikio yake na
kuyahifadhi kwa muda ili ayatafakari kabla hayauruhusu moyo wake
kuyatafrisi.
Wataalam wa masuala ya mahusiano wanashauri kuwa lugha ya mwili (body
language) inaongea kwa sauti zaidi ya sauti yako. Hivyo, unapaswa
kujiweka vizuri tangu unapomuangalia, unapomsalimia, mwili wako unapaswa
kuongea kitu.
Hii inakuwa rahisi sana kama moyo wako umempenda kweli, mwili huongea wenyewe bila kuulazimisha.
Wanawake wengi wanajua kuzisoma lugha za mwili hata kabla ya lugha ya
sauti. Hata hivyo, mioyo yao huwa migumu kuamini kile wanachokiona au
kukisikia hususan kama wameshawahi kuumizwa mara kadhaa (kitu ambacho
kipo kwa wanawake wengi hasa warembo).
Hata hivyo, baadhi hujikuta wanakupa nafasi ya kukusikiliza baada ya
kugundua kuwa wewe unaonesha kupenda kweli tangu machoni. Imani ambayo
huwepo kwa muda tu huku wasiwasi wa kuwa huenda unadanganya unakuwa juu
zaidi.
Maneno na vitendo vyako vitakusaidia sana katika kuuteka moyo wa
msichana unaetaka kuanzisha nae uhusiano ‘serious’ hivyo yachague kwa
umakini. Tumia muda fulani mdogo kumsoma anachopenda, story anazopenda
kuongelea na sehemu anazopenda kutembelea. Fahamu pia aina ya filamu
anazopendelea na mengine ili uweze kuwa aina ya mwanaume unayeweza
kucheza kila ngoma atakayokupigia katika mtiririko wa maisha.
Utafiti huo utakurahisishia maisha, na endapo utakaa naye vizuri na
uhusiano wenu unaweza kuanza hata bila kumwambia maneno mengi. Yaani
vitendo vikaongea hata bila kutumia maneno yanayotafsirika kama
‘kutongoza’. Kitakachofuata ni kumwambia maneno machache ili asikie
alichokuwa anataka kusikia kutoka kwako. Funguka, na mwambie kiunaga
ubaka.
Post a Comment