Waziri
wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu
amesema ugonjwa wa Corona unaelekea kuisha nchini ambapo mikoa zaidi ya
15 haijaripoti mgonjwa yeyote wa Corona kwa zaidi ya wiki.
Waziri
Ummy amesema hayo leo wakati alipotembelea kituo cha afya cha Mkonze
kilichotengwa kwa ajili ya kuwahudumia watu waliopata maambukizi ya
ugonjwa wa Corona jijini Dodoma na kukuta vitanda vikiwa tupu bila kuwa
na mgonjwa yeyote kwa zaidi ya wiki.
Waziri
Ummy amesema kupitia Waganga wakuu wa Mikoa 15 nchini wamethibitisha
kutokua na mgonjwa wa Corona na Mikoa mingine yenye wagonjwa imeripoti
kuwa wagonjwa hao wanaendelea vizuri.
Aidha,
Waziri Ummy amewashukuru watoa huduma za afya wa kituo cha Mkonze kwa
kazi nzuri walioifanya ya kuwahudumia wagonjwa na kuchukua tahadhari
zilizosaidia wahudumu hao kutopata maambukizi ya Corona.
Pamoja
na hayo Waziri Ummy amesema licha ya ugonjwa wa Corona kuelekea
kumalizika nchini, amewataka wananchi kutobweteka na kuendelea kuchukua
tahadhari kwa kuzingatia maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya
ikiwemo kunawa mikono mara kwa mara kwa sabuni na maji tiririka pamoja
na kuvaa barakoa za vitambaa wanapokua kwenye mikusanyiko
Post a Comment