Hii mara nyingi inatokea kwa wanawake, Dada zangu nadhani mna kaugonjwa, ukimpenda mwanaume, akakujali akakuthamini na kuonyesha upendo ule wa kwenye TV, kwanza unamuamini, pili baada ya kumuamini, awe ni mume au mpenzi basi unataka awe na maisha bora, yaani badala ya kuwaza wewe ufanikiwe uwe na maisha bora unataka mume wako au mume mtarajiwa awe bora.
Hapa unaanza kujitoa, unasahau maisha yako, unaanza kuishi
yake. Unachukua mkopo mnajenga katika kiwanja chake ambako alinunua
kabla, si unamuamini, unaacha kazi kulea familia, si ana kipato
atahudumia, unaanza kusimamia miradi yake, yaani badala ya kuwaza namna
ya kaunzisha miradi yako, ufanikiwe kama wewe unajisahau kabisa, unakua
unasimamia miradi yake.
Tena wakati mwingine unakua mkali sana kwenye mali zake kuliko hata
yeye, unasahau kua hata kama kakuoa ni zake, hata mkija kugawana kama
hujui kutafuta zako unajua kutafuta zake utaumia. Unajisahau, huna kitu
cha maana, unafanya kazi kila siku ni kumshauri kwanini usinunue
kiwanja, kwanini usifanye hivi, unamshauri mambo mengi ambayo wewe
hufanyi hata moja.
Huamini, hembu leo angalia wewe na mpenzi wako au mume wako, jiulize ni mambo gani unamshauri na namna unavyomsaidia yeye kufanikiwa. Halafu jiulize je kuna unachojishauri katika hayo mambo? Vipi wewe umefanya nini? Wengine utawasikia wakilalamika kabisa, mpenzi/mume wangu hataki kufanya vitu vya maendeleo, nikimshauri hataki anakalia pombe tu na starehe!
Swali ni je wewe unafanya vitu gani vya maendeleo, huna kazi kwanini wewe usianze kujishauri ukatafuta kazi kwanza kabla ya kumshauri yeye anunue kiwanja, jiangalie tu! Sasa unapoachana na mtu ambaye umetumia muda mwingi kumshauri mpaka akafanikiwa, nawewe ukajiona kama sehemu ya mafanikio halafu anakuacha utaumia sana.
Kwamba mbali na kuumia kuachwa na kupotezewa muda lakini unaumia kuwa huna cha maana ulichokipata, wakati yule ulityemshauri na kusimamia biashara zake atabaki na biashara, nyumba na kila kitu chake, wewe utaondoka na begi lako la nguo na maumivu ukiishia kulalamika na kusema namuachia Mungu! Ndugu yangu laana yako haifiki popote kwani ni wewe mwenyewe umeamua!

Post a Comment