Mfalme Salman wa Saudi Arabia amewahimiza viongozi wa nchi zilizoendelea kiviwanda na zinazoinukia kiuchumi, zinazounda kundi la G20, kuchukuwa hatua za ushirikiano na zenye tija, kutafuta majibu kwa mzozo wa kidunia unaosababishwa na mripuko wa virusi vya corona.

Aidha mfalme huyo amezitaka nchi wanachama wa G20, kuzisaidia nchi zinazoendelea. Wakati nchi tajiri kama Marekani zimetangaza mipango ya mabilioni ya dola ya kuupiga jeki uchumi, bado hakuna hatua zozote za pamoja zilizotangazwa na kundi la G20, ambazo zimekuwa zikikosolewa kwa kujivuta katika kutafuta sukuhisho.

Wito wa mfalme Salman umetolewa katika risala yake ya kuufungua mkutano wa kilele wa G20 ambao unafanyika kwa njia ya vidio leo Alhamis.

Amesema mzozo wa kibinadamu unaoendelea unahitaji suluhisho la kidunia, na kuongeza kuwa macho ya ulimwengu yanawatazama viongozi wa nchi wanachama wa kundi hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post