Hatimaye Kocha mwenye mataji mengi zaidi katika historia ya Liverpool na mwenye mafanikio makubwa, Bob Paisley amejengewa sanamu lake nje ya uwanja wa Anfield kama ilivyokua kwa mtangulizi na Boss wake, Bill Shankly.

Huyu ndiye binadamu ambaye ameishi zaidi Anfield kuliko mwingine yeyote. Tokea mwaka 1939 hadi 1983 akianzia kama mchezaji kisha baadaye akawa mtaalamu wa physiotherapy kabla ya kuwa Kocha msaidizi kufuatia ujio wa Bill Shankly.

Amebeba zaidi ya vikombe 20 akiwa na Liverpool kama kocha vingi kuliko mtangulizi wake Shankly na kutokana na mafanikio hayo amekua akitajwa kama kocha bora wa muda wote kwenye soka la Uingereza.

Kama hujui Paisley ni miongoni mwa makocha watatu ( Yeye, Zidane na Ancellot) ambao wamefanikiwa kushinda mara tatu taji la Ligi ya Mabingwa barani Ulaya UEFA.

Sifa Kuu ya Paisley ni kocha ambaye alikua akiingia ndani ya uwanja na kuwabeba mgongoni wachezaji wake pindi wanapoumia na sanamu alilojengewa limebeba picha halisi ya Bob jinsi alivyokua akiwabeba wachezaji wake.

Ukitazama kushoto mwa hilo sanamu utamuona King Kenny Dalglish mchezaji mwenye heshima zaidi kuwahi kucheza Liverpool akiwa na Iron Rush ambaye ni mfungaji bora wa muda wote Anfield. Hawa wamefundishwa pia na Paisley.

Pamoja na ukweli kwamba Bill Shankly ndie binadamu mwenye kuheshimika zaidi Anfield lakini ni wazi mafanikio yake yote yalitokana na Paisley ambaye alikua akitajwa kama ubongo wa Bill kwenye benchi la Liverpool lililokua likiundwa na Bill Shankly, Paisley, Joe Fagan na Ruben Bennet kukamilisha BOOT ROOM TRADITION.

NI ZAMU YA KLOPP

Nje ya uwanja wa Anfield sasa kuna sanamu mbili za makocha walioifanyia makubwa Liverpool.

Ya kwanza ni ya Bill Shankly ambaye yeye ndie msingi wa mafanikio na historia yote inayozungumzwa Liverpool leo.

Huyu ndiye mwanzilishi wa kile kibao cha This is Anfield ambacho wachezaji na benchi la ufundi ukigusa kila wanapokua wakiingia uwanjani kikiwakumbusha ukubwa wa Klabu waliyopo.

Ndiye aliyetoa wazo la kuufanya wimbo wa You'll Never Walk Alone kuwa wimbo rasmi wa Klabu. Na leo unatajwa kama wimbo maarufu zaidi kwenye Soka.

Yapo makubwa mengi ambayo Bill kayafanya kama tukisema tuandike yote tutajaza kitabu.

Sanamu la pili ni hilo la Paisley ambalo limezinduliwa jana na Mtendaji Mkuu wa Klabu, Bw Peter Moore. Huyu nimeshaeleza kwanini kajengewa sanamu.

Narudia tena. Ndiye binadamu alieishi zaidi Liverpool (miaka 44). Na ndiye kocha mwenye mafanikio zaidi Anfield.

Msimu huu ni wazi Liverpool wanaenda kushinda taji la England baada ya kitambo cha miaka 30 kupita.

Wapo kileleni mwa msimamo wakiwa na alama zao 70 baada ya kucheza michezo 24 na kushinda 23 huku wakidroo mchezo mmoja. Hivyo kwenye alama 72 ambazo walitakiwa kuwa nazo wameachia mbili tu.

Imebaki michezo 14 Ligi imalizike na wao wanahitaji kushinda michez o nane tu ili kutangazwa kuwa mabingwa wapya wa EPL baada ya kipindi chote hicho walichopitia.

Wapo moto. Hakuna anaetamani kukutana nao, wamefunga timu zote za EPL mpaka sasa. Guardiola mwenyewe kakiri ugumu wa Liverpool msimu huu.

Mafanikio yao yote yanatokana na ubongo wa Jurgen Klopp. Miwani yake mbele ya macho yake akiwa katika kizimba cha kusimama makocha (demarcation zone) kimekua kikiona mara mbili ya kile wanachoona makocha wa Timu pinzani wanaekutana nae.

Ameyaishi maneno yake aliyoyatoa Oktoba 2015 wakati alipotambulishwa kuwa kocha wa Liverpool. Alisema anaenda kuwafanya wale waliokua hawaamini kuhusu Liverpool waamini tena. Ni kama alitumia falsafa kufikisha ujumbe wake.

Haya yalikua maneno ya kufanana na Yale ya Alex Ferguson miaka 40 iliyopita alipokua akitambulishwa kuinoa Manchester United ambapo alisema anakuja kuvunja utawala wa Liverpool. Sasa Klopp yeye alitumia sanaa ya maneno kukisema kile kile kil…

[7:50 AM, 1/31/2020] Charles Dodoma: Viongozi mbalimbali wa Liverpool wakiongozwa na Mtendaji Mkuu wa Klabu hiyo, Bw Peter Moore (wa kwanza kulia) wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya sanamu la Kocha wa zamani wa Klabu hiyo, Bob Paisley lililozinduliwa jana kuonesha kuthamini mchango ambao kocha huyo aliutoa Anfield.

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp akishangilia ushindi wa Timu yake katika moja ya michezo ya Ligi Kuu.

Post a Comment

Previous Post Next Post