CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinatarajia
kushinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao kwa sababu ya mambo zaidi ya
nane waliyoyafanya katika jamii na yanaonekana hadharani.
Akizungumza
juzi jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa vijana wa Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam tawi la Abiyani, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James alisema katika uchaguzi huo njia ipo
nyeupe na wana uhakika wa kuchinja jogoo na kumla mapema bila ya kutoka
jasho.
Alisema CCM inajivunia katika ukarabati
na ujenzi wa barabara, madaraja, Hospitali, elimu na mengineo hivyo
hawana haja ya kujinadi kwakuwa jamii imewaelewa huku akiwabeza
wachambuzi wanaotumia fursa mbalimbali kukiponda chama hicho na viongozi
wao.
“Inashangaza sana kuna watu kwenye
shughuli za chama hawapo, kujenga chama hawapo, kukiimarisha chama
hawapo lakini kwenye uchambuzi hawajambo, hili ni jambo la kijinga sana
huwezi kuwa mchambuzi wa kisiasa bila kuwa na misingi au
taaluma,”alisema James
Alisema wakiendelea
kuwasikiliza wachambuzi hawawezi kufika popote kinachotakiwa ni kila mtu
afanye kwa chaguo lake huku akiwaonya kutokubali uchambuzi kwa watu
wasiowajua.
Alisema kwa mwaka huu wamedhamiria
kupambana na rushwa hivyo wale watao rushwa watakwenda na maji kwani
vitendo hivyo havina msamaha ndani ya chama,
Alisema wamedhamiria kufanya hivyo ili kutoa fursa hata kwa watoto wa maskini kuweza kupata uongozi kupitia CCM.
James
alisema ni vema vijana wakatumia nafasi waliyonayo kukijenga chama
kwani sifa kubwa ya uteuzi ni kuwaibumtsa wale waliokijenga au mateso
kwa chama na nchi pia.
Alisema haitakiwi
kuishi kwa kupiga ngoma au elimu kutafuta viongozi bora hivyo ni vema
kukijenga chama ili nacho siku moja kukijenga.
Watu wengi wanapotea baada ya chuo kutokana na kukosa marafiki sahihi na ushirikiano na watu walio nje ya chuo alichosoma.
Naye Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, alisema wanatarajia kushinda majimbo yote 10 katika jiji hilo.
Alisema
wamejipanga vilivyo kuanzia ngazi za matawi kuhakikisha wanashinda
nafasi zote kwa Dar es Salaam kwa kuwa wana mfumo mzuri .
“Tumekwisha
chinja jogoo wote ili kuua vizazi vya vifaranga hivyo tunatarajia
kukabidhi majimbo kumi yote ya mkoa wa Dar es Salaam,”alisema Kilakala
Post a Comment