NA Heri Shaban, ILALA
CHAMA Cha Mapinduzi( CCM ) Wilaya ya Ilala kimekibwaga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika nafasi ya Naibu Meya Ilala.
Katika uchaguzi huo CCM walimsimamisha Ojambi Masaburi aliyeibuka kidedea kwa kula 33 dhidi ya ya Elen Ryatula wa Chadema aliyepata kura 21.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo Msimamizi wa Uchaguzi Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilala Jabir Makame amesema kuliwa na wajumbe 57 na kati ya hao waliopiga kura ni 54.Hakuna kura iliyoharibika katika uchaguzi huo na uchaguzi huo umefanyika katika hali ya tulivu.
Akizungumza katika uchaguzi huo mara baada kuteuliwa Naibu Meya Mteule Manispaa ya Ilala Ojambi Masaburi amewapongeza wapiga kura kwa kumchagua kushika wadhifa huo.Pia amewapongeza viongozi wa CCM Wilaya kwa kumteua kwa kumpa tiketi ya CCM kugombea kiti hicho.
"Nashukuru kwa ushindi mnono uliotokana na madiwani wenzangu wa CCM kunichagua katika kiti hichi.Pia nawapongeza UKAWA kwani madiwani wake watano wamenipigia kura,"amesema Ojambi na kuongeza utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi unaofanyika chini ya Mwenyekiti wao Rais John Magufuli umefanya hata upinzani nao kuunga mkono na ndicho ambacho wamekionesha kwa kumpa kura.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ilala Jumanne Shauri ,awali alifungua kikao cha Baraza la madiwani Ilala alisema kikao hicho ni cha kawaida ,uchaguzi wa Naibu Meya kila baada ya mwaka mmoja .
Shauri amesema wapiga kura wajumbe wa kuteuliwa au kupiga kuratatibu Meya Mwenyekiti,Mkurugenzi Katibu utaratibu wa ushindi wa kiti mgombea anatakiwa kupat kura zaidi zilizopigwa na wajumbe.
Kwa upande wake Meya wa Ilala Omary Kumbilamoto amechagua kamati zake za kufanya nao kazi ambazo ni Kamati za Mipango Miji na Mazingira na Kamati na Kamati za Huduma za Jamii.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Ojambi Masaburi akizungumza katika Baraza la madiwani Arnatogluo leo (Picha na Heri Shaaban)
Mkurugenzi wa Halmashauri ya,Ilala Jumanne Shauri akisoma taarifa katika uchaguzi wa Naibu meya wa Ilala leo (Picha na Heri Shaaban)
Post a Comment