Licha ya Kuwa na Mke wa Ndoa, Akon Aendelea Kujiachia na Michepuko



Licha ya kuwa na mke wa ndoa kisheria Akon (50) bado ameendelea kugawa waziwazi muda na kuwapa airtime ya kimapenzi wanawake zake wengine (michepuko).


Siku chache zilizopita Akon alikuwa nchini Senegal kusherehekea birthday ya Ammirah mwanamke wake ambaye pia ni mwanamuziki, Amirrah amepost picha wakiwa pamoja kama kawaida yake anavyofanya mara kwa mara.


Kabla ya kwenda Senegal, Akon alikuwa Dubai kula maisha na mwanamke wake mwingine anayeitwa Rozina ambaye nae ameachia mapichapicha wakiwa pamoja Dubai na wote hao anawaita wake zake ingawa inaelezwa hajawaoa rasmi na bado ana wanawake wengine anaowaita girlfriends.


Ingawa mwanamuziki huyo wa Marekani anayetokea Senegal, ana mke mmoja anayetambulika kisheria. mkewe rasmi anaitwa Tomeka Thiam(48) aliyevaa nguo ya bluu pichani, ambaye walikutana enzi hizo Akon akiwa na miaka 20 na Tomeka akiwa na miaka 18. Wamejaaliwa kupata watoto 5 katika ndoa yao mtoto wao wa kwanza akiwa kazaliwa 1996


Akon ana watoto wengine 4 aliozaa na wanawake tofauti hivyo kiujumla Akon ana watoto 9.


Akon anasema haamini dhana ya mwanaume kuwa na mke mmoja hivyo anaona hata mataifa ya Ulaya na Marekani yanapaswa kuiga mataifa ya Afrika yenye utamaduni wa wanaume kuoa mke zaidi ya mmoja. Akon anaamini kazi ya mwanamke ni kukaa nyumbani kulea watoto huku mume akiwa ndio mtafutaji.


Lakini hata hivyo, Akon mwenye utajiri wa zaidi ya shilingi bilioni 149.7 za Kitanzania ($60 million), hivi karibuni alisema yeye ndie mwanaume bahili zaidi duniani huwa hatapanyi pesa ovyo ovyo au kuwa na matumizi mabaya ya pesa.


Mke rasmi wa Akon kisheria ni huyo mwenye nguo ya blue pichani ambaye ana miaka 48, mwenye nywele za rangi ya chungwa ni Ammirah na mwenye gauni la kijani na nyeusi ni Rozina.

-------------------

Post a Comment

Previous Post Next Post