Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imefungua majalada 23 ya kesi za rushwa ya ngono, kumi kati ya hizo zikisikilizwa na tano kushinda katika mikoa mbalimbali.
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), imefungua majalada 23 ya kesi za rushwa ya ngono, kumi kati ya hizo zikisikilizwa na tano kushinda katika mikoa mbalimbali.
TAKUKURU
pia, imewataka wakuu wa vyuo kusimamia suala la rushwa ya ngono vyuoni
ili kusaidia kupunguza ukandamizaji unaofanywa hususani kwa watoto wa
kike.
Hayo
yamesemwa Juni 18,2020 jijini Dodoma na mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya
kuzuia na kupambana na rushwa nchini,Brigedia Jenerali John Mbungo
wakati akifungua warsha ya utafiti wa rushwa ya ngono katika taasisi za
elimu ya juu ,uchunguzi wa kifani wa vyuo vikuu vya Dar Es Salaam na
Dodoma iliyoandaliwa na Taasisi ya kiraia ya Mfuko wa Wanawake
Tanzania[Women Fund Tanzania] .
Brigedia
Jenerali Mbungo amesema kufuatia kuwepo kwa malalamiko ya rushwa ya
ngono Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini [TAKUKURU]ilitoa
tamko la kushughulikia taarifa za malalamiko ya rushwa ya ngono ambapo
kuanzia mwaka 2013 hadi machi 2020 jumla ya majalada 23 yalifunguliwa
kwa mikoa 14 ya Tanzania.
Brigedia
Mbungo amesema mkoa wa mwanza majalada 4 Yalifunguliwa,majalada 3 kwa
kila mkoa katika mikoa mitatu ya Kagera,Mtwara na Mara na jalada 1 kwa
kila mkoa katika mikoa 10 ya Arusha,Dodoma ,Geita,Iringa
,Katavi,Kinondoni,Manyara,Rukwa ,Singida na Temeke.
Aidha.Brigedia
Mbungo amesema jumla ya kesi 10 zilizofunguliwa Mahakamani,kesi tano
zishinda na kati ya hizo nne zilihusu taasisi za Elimu,kesi 3
zilishinda kesi moja iliondolewa mahakamani na kesi moja inaendelea
Mahakamani ambapo majalada 10 yanaendelea na uchunguzi ambapo katika
jitihada za kudhibiti rushwa ya ngono TAKUKURU kwa kushirikiana na Mfuko
wa Wanawake Tanzania wamezindua kampeni ya Vunja Ukimya kataa rushwa ya
ngono .
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya mfuko wanawake (WFP) Prof.Ruth
Meena amesema kuwa Pamoja na jitihada kubwa inayofanywa na Serikali
kuwalinda watoto wa kike bado wanakabiliwa na kupewa vitisho wanapotaka
kujinasua katika rushwa ya ngono.
Naye
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Door of Hope Tanzania Clemente
Mwombeki amesema kuwa Jamii bado haina uelewa juu ya madhara ya
rushwa ya ngono hali inayokwamisha juhudi za wanaharakati Katika
kufuatilia ukatili huo.
Mwanasheria
wa TAKUKURU kupitia Idara ya Uzuiaji Rushwa Denis Lekayo amesema
kumekuwepo na baadhi ya wanawake kutengeneza mazingira ya kushawishi
rushwa ya ngono .
Post a Comment