Rais
wa Tanzania, Dr John Magufuli amesema atafungua shule za msingi na
sekondari hivi karibuni, kama ataridhishwa na kasi ya upunguaji wa
maambukizi ya ugonjwa wa Corona
Rais
Magufuli amesema hayo leo Ijumaa tarehe 5 Juni 2020, wakati akifungua
mkutano mkuu wa uchaguzi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), jijini
Dodoma.
Amesema,
maambukizi ya corona yamekuwa yakipungua siku hadi siku huku akiendelea
kuwasisitiza wananchi kuchukua tahadhari ya ugonjwa huo.
Huku akishangiliwa na umati wa mkutano huo, Rais Magufuli amefurahishwa na washiriki wa mkutano huo walioujaza uwanja wa Jamhuri, Dodoma kutokuvaa barakoa huku akionyesha kushangazwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai kuvaa barakoa akiwa ndani ya Bunge.
“Corona imekwisha ndiyo maana hata mabarakoa hakuna, hata leo tunaonana tu hapa kawaida, ndiyo maana nilikuwa namshangaa Spika Ndugai akiwa Bungeni yupo kiti chake peke yake lakini amelivaa hilo libarakoa mdomoni, Watanzania tumtangulize Mungu."-Amesema

إرسال تعليق