KAIMU Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', Ettiene Ndayiragije amesema bado timu ya Taifa ina nafasi ya kupata matokeo mbele ya Kenya.

Kwenye mchezo wa kwanza wa kutafuta tiketi ya kushiriki michuano ya Chan inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon, 2020 uliochezwa uwanja wa Taifa Stars ilikubali kupata sare ya bila kufungana.

Ndayiragije amesema:"Uwezo wa wachezaji unakua mkubwa kila leo na wanatambua kwamba wana kazi kubwa ya kufanya nchini Kenya hasa baada ya mchezo wa kwanza kutopata matokeo.

"Makosa yetu yalikuwa ni kwenye kumalizia nafasi ambazo tumezitengeneza jambo ambalo tumelifanyia kazi hivyo tunakwenda ugenini tukiwa na imani ya kushinda, mashabiki watupe sapoti," amesema.

Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Agosti 4 nchini Kenya na ili kufuzu michuano hii ni lazima Stars ishinde.

Post a Comment

أحدث أقدم