Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mvua zinazoendelea kunyesha mfululizo zimeanza kusababisha hofu ya kuleta madhara katika maeneo mbalimbali mkoani Lindi.
Habari kutoka katika kijiji cha Njinjo, wilayani Kilwa zimeeleza kwamba maji yanatoka mto Matandu yameanza kuingia majumbani. Hali ambayo imeanza kusababisha taharuki na hofu kwa wananchi.
Mtendaji wa kijiji hicho, Yahya Mketo amethibitisha. Baada ya kuulizwa na Muungwana Blog kuwepo hali hiyo katika kijiji hicho kilicho jirani na mto Matandu.
Mketo amesema maji hayo yalianza kufika na kuingia kwenye makazi ya watu, leo kuanzia majira ya saa tisa mchana.
'' Nikweli ipo hali hiyo, lakini bado mpaka sasa hakuna madhara yaliyotokea,'' alisema Mketo.
Ofisa mtendaji huyo amebainisha kwamba wananchi, hasa walio maeneo ya bondeni wameondoka na kwenda kujihifadhi kwa ndugu zao ambao nyumba zao hazipo bondeni.
'' Tumewaambia waondoke, kwani hatujui hali ya usiku huu itakuwaje. Mimi mwenyewe nitabaki maeneo aya usiku wote, kuwapa taarifa wananchi kila kitakacho endelea.
Tumeweka na alama ili kuona kama yataongezeka au kupungua,'' aliongeza kusema Mketo.
Juhudi za kumpata mkuu wa wilaya ya Kilwa, Chritopher Ngubiagai zinaendelea ili kupata taarifa za kina kuhusu taarifa hiyo na zamaeneo mengine wilayani humo.
Post a Comment