Watu 350 wapimwa na kukutwa na virusi vya corona katika mataifa 28 barani Afrika.
Benin na Tanzania zatangaza kesi yake ya kwanza kila mmoja tangu kunza kwa janga hilo mwishoni mwa mwaka 2019.
Bara la Afrika hadi wiki iliopita ilikuwa bado imenusurika na virusi hivyo hadi kesi chache kuanza kuripotiwa .
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO limetangaza Jumatatu kuwa
barani Afrika katika mataifa 28 ni watu 350 ndio waliokutwa na virusi
vya corona baada ya kupimwa.
Nchini Benin, mtu wa kwanza kukutwa na virusi hivyo ni mwanamume mwenye
umri wa miaka 49 na raia wa Burkinafaso ambae aliwasili nchini Benin
Machi 12.
Tanzania imetangaza mtu wa kwanza kuwa na virusi hivyo huku mataifa
jirani yakitangaza pia kuchukuwa hatua zinazostahili kuzuia kujipenyeza
kwa virusi hivyo.
Mtu huyo aliekutwa na virusi ana umri wa miaka 46 aliwasili nchini Tanzania akitokea nchini Ubeligiji Machi 15.
Rwanda imetangaza kesi 6 mpya kwa muda wa masaa 48.
Wizara ya afya ya Rwanda amefahamisha kuwa mmoja miongoni mwa waathirika ana umri wa miaka 30 na mkazi wa jiji la Kigali .
Afrika Kusini ndio taifa lililoathirika kwa kiasi kikubwa barani Afrika na wagonjwa 51 baada ya Misri yenye wagonjwa 126.
Rais wa Afrika Kusibi Cyrille Ramaphosa ametangaza kusitishwa kwa
safari kutokea katika mataifa yenye tishio kubwa la Covid-19 kama
Italia , Ujerumani, China na Marekani.
Post a Comment