Ukosefu
wa huduma ya Maji safi na Salama kwa Wakazi kata ya Ngogwa katika
Halmashauri ya Mji wa Kahama mkoani Shinyanga umetajwa kuhatarisha
Maisha ya wanawake kutokana na baadhi yao kujeruhiwa na wanyama aina
ya fisi pindi wanapokwenda kuchota maji kwenye visima vilivyopo umbali
wa kilomita 6 nyakati za alfajiri.
Kauli
hiyo imetolewa June 5 Mwaka huu na Diwani wa Kata ya Ngogwa,Kamuli
Mayunga wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya
Wilaya ya Kahama iliyotembelea Mradi wa Maji Safu wa Ngogwa-Kitwana
unaojengwa na Mamlaka za Maji, SHUWASA, KUWASA na RUWASA.
Alisema
kuwa Kumekuwa na Matukio mengi ya wanawake kushambuliwa na wanyama hao
ambao wanapatikana kwa wingi katika eneo hilo kutokana na kuwepo kwa
milima mingi na kusema kuwa kukamilika kwa mradi huo utaweza kutokomeza
matukio hayo sambamba na magonjwa ya homa za matumbo.
“Tunashukuru
ujio wa Mradi huu miaka miwili iliyopita tulipoteza wanawake wawili kwa
kushambuliwa na fisi hadi kufariki dunia wakati wakienda kuchota Maji
nyakati za alfajiri,Tunaipongeza serikali kwa kusikiliza kero hii ya
kumtua mama ndoo kichwani,”alisema Kamuli.
Celina
Paulo ni Mkazi wa kijiji cha Nyamela alisema kuwa fisi wamekuwa kikwazo
kwao pindi wanapokwenda kuchota Maji asubuhi na kuiomba Serikali
kuhakikisha wanakamilisha Mradi huo kwa wakati ili kuwaondolea adha hiyo
ili kundelea na shughuli zingine za uzalishaji Mali.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa
Mazingira Shinyanga (SHUWASA) Flaviana Kifizi alisema Mradi huo
umekamilika kwa asilimia 95 na utagharimu shilingi bilioni 2.4 na
utakamilika mwezi Agosti Mwaka huu na unatarajia kunufaisha zaidi ya
wakazi 1000 wanaoishi pembezoni mwa Halmashauri hiyo.
“Ujenzi
wa Matanki Mawili ya Ngogwa na Kitwana umekamilika na kwa sasa
tunatarajia kuanza kulaza mabombo ili kuruhusu maji kuanza kutumiwa na
wananchi,pia tutajenga vituo 13 vya kuchotea maji ambayo yatawawezesha
wananchi kupata huduma za maji safi na salama ambayo itakuwa suluhisho
la wao kutembea umbali Mrefu kutafuta huduma hiyo,”alisema Kifizi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa wilaya ya
Kahama,ambaye ndio Mkuu wa wilaya hiyo Anamringi Macha alisema kuwa
serikali ya awamu ya Tano Chini ya Dk John Pombe Magufuli imedhamiria
kitatua kero zote za wananchi hususani ya Maji kwa kuhakikisha wanapata
maji safi na salama.
“Katika
mradi huu niwaombe wananchi msiweke vikwazo pindi watakapoanza kuchimba
mitaro ya kupitisha Mabomba kwani hakuna mtu atakayelipwa fidia,tutoe
ushirikiano ili kufanikisha mradi huu kwa wakati na tuendelee na
shughuli za uzalishaji maji kupita huduma ya maji,”alisema Macha.
Post a Comment