Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini imetoa ufafanuzi juu ya uwepo wa vipindi vya mvua ambapo imesema zinatokana na mgandamizo mdogo wa hewa katika eneo la bahari ya hindi .
Taarifa iliyotolewa na mamlaka hiyo leo,Oktoba, 13, inadai kuwa mvua hizo zitapungua siku ya kesho tarehe 14/10/2020 na kuongezeka tarehe 15/10/2020.
Aidha Mamlaka hiyo imewataka wananchi kuzingatia tahadhari zinazotolewa na miongozo kutoka katika wataalamu wa sekta husika ilikupunguza athari zinazoweza kujitokeza.
Hata hivyo mvua za Vuli katika maeneo ya Pwani Kaskazini na nyanda za juu Kaskazini mashariki zinatarajia kuanza kati ya wiki ya pili au tatu ya mwezi Novembaza Oktoba na Disemba 2020 kama zilivyotabiriwa hapo awali
Post a Comment