Na Faruku Ngonyani, Mtwara

Mkuu wa Wilaya ya Newala iliyopo Mkoani Mtwara Aziza Mangosongo amekasirishwa na matokeo mabovu ya mtihani wa darasa la Saba (7) ya Shule ya Msingi Mikumbi baada ya kufaulisha wanafunzi (3) kati ya 63 waliofanya mtihani huo.


Mkuu huyo wa Wilaya amesema kuwa Shule hiyo kwa sasa imeshika nafasi ya mwisho kimkoa huku ikiwa nafasi za chini kabisa kitaifa.


Aidha Dc Aziza ameelezea kuwa moja ya sababu zilipelekea wanafunzi hao 60 kufeli ni pamoja na baadhi ya wazazi kuwashawishi watoto wao waandike majibu ya uwongo ili  wafeli na wasiingie gharama za kuwasomesha.


Kwa nafasi hiyo Mkuu huyo wa Wilaya ametoa agizo kwa wazazi na walezi wa wanafunzi wote 60 waliofanya vibay mitihani hiyo a kuhakikisha wanawapeleka  watoto hao vyuo vya ufundi ili wakapate elimu ya ujuzi.


“Mikumbi Shule ya msingi mmetutia aibu kubwa mnoo,Kitafa tupo chini yaani tukisema chini yaani hata nafasi ya ishirini kule chini hatujafikia lakini Kimkoa ndio shule ya mwisho kwenye kufaulu yaani kati ya wanafunzi 63 waliofaulu wa 3 tu basi”Dc Mangosongo


“Na kwa taarifa ambazo ninazo kuna wazazi mliwaambia watoto wenu wafeli unamwambia akaandike makorocho ili  mtoto afeli ,sas kama ulimwambia mtoto afeli ili akifaulu usipate majukumu ya kutafuta daftari au yunifomu  hamna mlichokifaya, sasa watoto wote hawa waende shule kwa gharama zenu na nitahakikisha watoto wote hawa wananenda shule”Dc Mangosongo

Post a Comment

Previous Post Next Post