Na Timothy Itembe Mara.

MWENYEKITI wa Chama cha mapinduzi na Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania DK,Samia Suluhu Hassani amepongezwa kwa kuleta fedha zaidi ya kiasi cha shilingi Bilioni 420 za kutekeleza miradi ya kijamii mkoa Mara.


Kauli hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mara,Patrick Chandi mbele ya kongamano la tathimini ya miaka miwili ya utekelezaji wa shughuli za miradi ya DK,Samia Suluhu Hassani Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania ambalo liliandaliwa Mwenyekiti huyo alisema fedha kutekeleza miradi. kwa miaka miwili ya Samia ni ahadi ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa Chama cha mapunduzi ya 2020-2025.


Chandi alisema CCM haina budi kujivunia mafanikio aliyoyafanya Rais Samia Suluhu Hassani kwa miaka miwili ambayo itawahakikishia kushinda kwa kishindo Wakati wa uchaguzi ujao wa serikali za mitaa 2024 na uchaguzi mkuu 2025.


"Mkataba wetu kwa wananchi , sisi tuwape maendeleo na wao watupe kura hatuna cha kulipa bali shukurani zetu za pekee mkoa wa Mara nikukipa kura Chama cha mapinduzi mwaka 2024/2025". alisema Mwenyekiti Chandi.


Mwenyekiti huyo alitumia nafasi hiyo kumuomba Rais kujenga reli ya Arusha-Mara ambayo utekelezaji wake ulianza mwaka 1998 hadi sasa haujaanza kutekeleza pia kumuomba wimbo huugawanya wilaya ya Serengeti kwa kuwa ni kubwa ili kuwa na majimbo mawili ya uchaguzi na kusogeza huduma za jamii karibu.


Kwa upande wa Mkuu wa mkoa wa Mara Meja Jen erali Seluiman Mzee alitoa taarifa ya miradi katika miaka miwili ya utawala wa Rais DK,Samia SuluHu Hassani katika sekta mbalimbali katika mkoa Mara ambapo alisema mafanikio yaliyopatikana yanalenga kuboresha maisha na huduma kwa wananchi.


Mzee alisema mkoa wa Mara umefanya kongamano la kuelezea umma juu ya utekelezaji wa majukumu ya kazi katika sekta mbalimbali zilizofanywa cha miaka miwili ya Rais wa awamu ya sita ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan ambapo alitaja moja ya miradi iliyotekelezwa pamoja na hayo. upatikanaji wa huduma ya maji ya RUWASA.


Zaidi ya miradi 52 yenye thamani ya zaidi yashilingi bilioni15.756 imetekelezwa pia zaidi ya vijiji 195 vimefikiwa na huduma ya maji kutoka asilimia 54 na kufikiria asilimia 71 ambayo kwa upande wake ufikiaji wa huduma ya huduma ya maji na maradhi hususani ugonjwa wa kichocho alisema Mzee. .


Katika hatua nyingine alisema mradi wa maji wa Mugango -kiabakari -Butiama ulioanza mwaka 2020 ambao ulitakiwa kukamilika februari 2022 umefikia asilimia 74 na utasambaza maji katika vijiji vya wilaya za Butiama na Musoma.


Katika sekta ya afya alisema mkoa huo umepokea zaidi ya bilio katika 36.176 kwa ajili ya kuboresha huduma za matibabu ya afya kwa wananchi ikiwa ni pamoja na manunuzi ya vifaa vya ujenzi wa zahanati,vituo vya afya sambamba na ujenzi wa mawodi mkoani hapa.


Mkuu wa mkoa alitumia nafasi hiyo Amewaomba kuwataka watumishi na viongozi mbalimbali kutuma ili kukamilisha miradi ambayo haijakamilika iweze kukamilika kwa wakati ili kujenga hoja ya kuomba fedha kwa ajili ya miradi mingine kama ujenzi wa Standi mpya ya kisasa ya mabasi ambayo haipo Mara.


Mzee alimaliza kwa kusema shilingi Bilioni 35 zimepokelewa TANRODS kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa Barabara ya lami uwekaji wa taa na matengezo ya mitaro.

Post a Comment

أحدث أقدم