Aliyemuua Mkewe TABATA Ahukumiwa Kifo


Mtanzania Alli Balanda Idofulo amehukumkwa kunyongwa hadi kufa na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam baada kupatikana na hatia ya kumuua Mkewe Selan Kondo.

Hukumu hiyo imetolewa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambayo imepewa mamlaka ya kusikiliza shauri hilo ambapo Kondo alituhumiwa kutekeleza mauaji hayo kwa kutumia kisu ambacho alimchoma Mkewe begani.

Katika hukumu hiyo iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Franco Kiswaga, Mahakama imejiridhisha pasi na shaka ya kwamba Kondo alimuua Mkewe kwa kumchoma na Kisu.

Hatua ya hukumu hiyo inatokana na Mahakama kujiridhisha na ushahidi wa Mashahidi wanane akiwemo Mtoto wa Marehemu mwenye umri wa miaka minane, ambaye aliieleza Mahakama kuwa aliishuhudia Kondo akimchoma kisu Mama yake baada ya kutokea msuguano baina yako.

Idofulo anadaiwa kumuua Selan Kondo, May 6, 2019 eneo la Tabata Liwiti, Wilaya ya Ilala, inadaiwa siku hiyo ya tukio, Mshtakiwa alimuita Kondo waonane ili wajadiliane namna ya kurudiana baada ya kutengana kwa muda mrefu.

Post a Comment

Previous Post Next Post