ERoni said:
Siku hizi Ke wakimalizana na Me wanategemea kupewa pesa, yaani wakitoka Lodge Ke anasubiri kupewa "kifuta jasho", kwa nini iwe hivyo?
Kawaida sikuwa na tabia hiyo, baada ya kumaliza tendo, nilimwacha aende zake, baada ya siku mbili angenitafuta na kuniomba pesa kwa visingizio vya hapa na pale, nami ningemtumia kwenye simu imfikie huko huko kwao! Mapenzi kidogo yanakuwa yenye discipline! Nilimkosea akashindwa kusamehe, kila mtu akapita njia yake!
Huyu niliyenaye kwa sasa simuelewi, mahusiano yetu hayajamaliza wiki tatu, hivyo hajaqualify kigezo cha kupajua kwangu! Ni mara ya pili nachakata! Lakini kila tunapomaliza anaanza kuisoma miondoko ya mikono yangu, nikiisogeza kwenye kingo ya kitanda na yeye anaelekezea macho huko huko, nikiingiza mfukoni, anaisindikiza kwa macho! Kibaya istoke na pesa, uso unachora X, mara ya kwanza sikumpatia pesa, aliondoka akiwa mnyonge! Baada ya siku mbili nilimtumia 40K kama kipozeo.
Mpinduko wa pili, baada ya kumaliza sikumpatia pesa, akaniuliza "kwa hiyo" Nikamwambia tutaonana siku nyingine, akasema,"Ndo hivyo basi" Nikachekea kimoyo moyo! Njia nzima ananifuata tu, mwisho wa siku anaanza kujisemesha mara "Kesho nikienda kumtazama mama hospitali niende walau na matunda ili aone umuhimu wa mimi mwanae, sijui ela ntapata wapi!"
Ingawa aliongea kwa hisia kali ila nilijua tu ni technic ya kupatiwa Kipozeo!
Kwani ni lazima kutoa kwa mpenzi ulie na mahusiano nae baada ya tendo?
Post a Comment