Ofisi ya Rais - TAMISEMI imesema imeona taarifa zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikimuhusisha Mwanafunzi Sifika Daniel Rubern aliyesoma Shule ya Sekondari ya Mkombozi iliyoko Wilaya ya Same, Kilimanjaro na kupangwa kidato cha tano Sekondari ya Namwai kuwa nafasi yake amepewa Mwanafunzi mwingine hivyo yeye kukosa haki ya kuendelea na masomo.


Taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini -TAMISEMI, Nteghenjwa Hosseah imesema “TAMISEMI imefuatilia taarifa hizo kwa kina kutoka Mkombozi Sekondari alikosoma Mwanafunzi huyo (O’level) mpaka Shule ya Sekondari Namwai alikopangiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano”


“Imebainika anayelalamika mitandoni anaitwa Sifaeli Tawel Elirehema na alisoma Shule moja na Sifika Daniel Rubern, hata hivyo Binti huyo namba yake ya mtihani ilikuwa ni S.850/135 alipata Div IV: 34 (Zero) na alisoma masomo ya Sanaa ilihali Sifika Daniel Ruben namba yake ya mtihani ni S.850/136 alisoma masomo ya Sayansi na amepata Division 1:10”



“Binti anayelalamika mitandaoni alifikishwa Shuleni hapo na Wazazi/Walezi kuripoti akiwa hana viambatanisho vyovyote (Result Slip) na alipohojiwa ilibainika kuwa amewadanganya Walezi wake kuanzia jina mpaka matokeo yake na kwasababu Walezo hao walimchukua kama Msaidizi wa nyumbani hawakufahamu ukweli wa taarifa walizopewa na Binti huyo.


Hakuna aliyenyang’anywa haki yake ya kuendelea na masomo ya kidato cha tano na taarifa zilizotolewa na Binti huyo ni za uongo na zipuuzwe na Mwanafunzi Sifika Daniel Ruben anaendelea na masomo yake.


Anayeonekana pichani ndiye Mwanafunzi Sifika ambaye jina, namba na picha yake vimetumika kudanganya umma na yeye ndio ambaye yuko Shuleni aliyepata Division one


“Wazazi/Walezi na wanaharakati msisambaze taarifa ambazo hamjajiridhisha na usahihi wake ili kuepuka kuzua taharuki kwenye Jamii.”

Serikali Yafunguka ishu ya Mwanafunzi Anayedaiwa Kuibiwa Matokeo


-------------------

Post a Comment

Previous Post Next Post