Enzi za Cristiano Ronaldo na Lionel Messi za kutawala tuzo za mpira zinaendelea kusukumwa ukingoni, na usiku huu beki wa Liverpool na Uholanzi Virgil van Dijk amewaangusha.

Van Dijk amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa bara Ulaya kwa mwaka 2018/19 Van Dijk baada ya kuingoza safu ya ulinzi ya Liverpool kuchukua Champions League msimu uliopita.

Kama Luka Modric alivyofanikiwa kuwaoondoa Ronaldo na Messi katika udhibiti wa tuzo hiyo mwaka jana - Van Dijk amekuwa mtu wa pili kuwapiku nyota hao ambao wametamba kwa zaidi ya muongo mmoja uliopita.



Post a Comment

Previous Post Next Post