MLIPUKO wa lori la mafuta nchini Uganda umesababisha vifo vya watu tisa na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Tukio hilo limetokea siku ya jana jioni katika kituo cha biashara cha Kyambura kilichopo Wilayani Rubirizi, Magharibi mwa Uganda.
Mkuu wa Wilaya ya Rubirizi, Harriet Nabukenya, alisema dereva wa lori la mafuta alishindwa kudhibiti mwendo wa lori hilo na kuvamia teksi mbili za abiria zilizokuwa zimeegeshwa barabarani, baada ya sekunde kadhaa lori hilo liliwaka moto.
Moto huo ulienea katika nyumba na maduka kadhaa na kuteketeza vitu. Onesmus Nkesiga ambaye duka lake lilikumbwa na moto huo, alisema amepoteza bidhaa zenye thamani ya USh 20 milioni.
Wazima moto ambao walifika katika eneo hilo saa moja baada ya tukio, wameokoa vitu kadhaa kwenye baadhi ya maduka.
إرسال تعليق