Waathiriwa wa kirusi cha corona nchini Kenya
wamefikia watu saba baada ya watu wengine watatu kuthibitishwa
kuambukizwa kirusi hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari leo
Jumatano, Waziri wa Afya wa Kenya, Mutahi Kagwe amesema kuwa, watu wote
hao saba wametoka nje ya Kenya. Wawili kati ya wagonjwa hao watatu wa
karibuni kabisa wametokea Madrid Uhispania kupitia Dubai na mgonjwa wa
tatu ni raia wa Burundi aliyewasili katika Uwanja wa Ndege wa Jomo
Kenyatta jijini Nairobi akitokea Dubai pia.
Huku hayo yakiripotiwa, Wizara ya Afya
ya Afrika Kusini imetangaza kuongezeka idadi ya waathiriwa wa kirusi cha
corona nchini humo na kufikia watu 85 ikiwa ni ongezeko la watu 34
ikilinganishwa na taarifa ya kabla yake.
Kabla ya hapo Wizara ya Afya ya Afrika Kusini ilikuwa imetangaza kuwa watu 51 wameambukizwa kirusi cha corona nchini humo.
Katika juhudi za kupambana na maambukizi
ya kirusi hicho hatari, viongozi wa Afrika Kusini wameziweka chini ya
karantini meli mbili karibu na Capetown, moja ni meli ya mizigo na
nyingine ni ya kitalii.
Meli ya kitalii kati ya hizo mbili ina abiria elfu moja na 240 na wahudumu 486.
Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini
ametangaza hali ya "Janga la Taifa" katika maeneo yote ya nchi hiyo
kufuatia kuenea kwa kasi maambukizi ya kirusi cha corona, ugonjwa ambao
jina lake rasmi na COVID-19.
Post a Comment