Wizara ya Afya imetangaza nafasi za ajira 1650 kwa wataalamu wa kada mbalimbali za afya nchini.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi Aprili 16, 2022 na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Profesa Abel Makubi imeeleza kuwa wizara hiyo imepata kibali cha kuajiri ambapo wataalamu hao wataajiriwa na kupangiwa vituo vya kazi ambavyo vipo chini ya uendeshaji wa moja kwa moja wa wizara hiyo.

Miongoni mwa nafasi hizo, zipo za madaktari bingwa (25), madaktari (215), wafamasia(15), maafisa maabara(62), wateknolojia (dawa, maabara, mionzi, macho-155), maafisa uuguzi (140), maafisa uuguzi wasaidizi (467), wauguzi (140), wakemia (2), madaktari wa afya kinywa na meno (15), tabibu meno (19), watoa tiba kwa vitendo (15), wazoeza viungo kwa vitendo(31), maafisa wazoeza viungo (33), maafisa afya mazingira(40), wasaidizi wa afya (134), wahandisi vifaa tiba (17), wateknolojia vifaa tiba (40) , watunza kumbukumbu wa wfya (10) na madereva (4).

 

Post a Comment

أحدث أقدم

ZAIDI